ULIVYOZUNGUKA MLIMA HUU VYATOSHA!!!!!!!!!!!!!



>>>>>>KUMBUKUMBU 2:1-3<<<<<<<<<<<<<<

Mpendwa,Inawezekana kabisa kuwa maisha yako yamekuwa ni ya kukatisha tamaa,Huoni hata mlango wa kuanzia wala hujui njia ya kuiendea.

Mungu ana NENO juu yako.Wana wa israeli walipokuwa wanaambiwa na Musa kwa habari ya ukombozi wao waliona kama anaongea habari za ndoto za mchana.Hawakuamini kuwa Mungu anaweza watoa kweli kwenye mikono ya Farao kwa jinsi alivyo kuwa na majeshi hodari.

Hata walipotolewa katika mikono ya Farao, wanapofika Bahari ya Shamu bado hawaamini kuwa wanaye mfanya njia pasipo njia mbele yao na mkausha bahari.Wanamlilia Mungu wakiwa na Musa.
KUTOKA 14:13-15.

KUMBUKA Musa ameshawaambia kuwa simameni mkauone wokovu wa Bwana. Mungu anamwambia Musa kwanini MNANILILIA mimi? Cha kushangaza ni kwamba na Musa alianza kulia.Jifunze kuwa huwezi ukapata ukombozi kwa IMANI ya mtu mwingine hata kama ni mtumishi.Yesu alikuwa anawaambia waliokuwa wanamwendea kuwa, “IMANI YAKO IMEKUPONYA”.

Mungu akasema waambie wana wa Israeli waendelee mbele.Sasa hapa lazima ujifunze kitu kuwa Mungu alikuwa anazungumza kwa habari za rohoni. Asingeweza kuwaambia kuwa waendelee mbele wakati mbele yao tayari ni bahari.Hapa anazungumza kwa habari ya Imani zao.

LAZIMA ulione tatizo lako kuwa limekwisha kupata suluhisho unapomwendea Mungu.Uwe na uhakika kuwa suluhisho lako unalo mkononi.Kama ambavyo mtu mwenye akaunti benki anapokwenda kuchukua fedha benki anakuwa na uhakika kuwa hela alizonazo benki atazipata La sivyo awe amekosea namba za siri(PASSWORD) za kadi yake.Hata kwako mpendwa lazima ujue ninamba ya siri ipi ya Mungu kukupa unacho mwomba.IMANI YAKO NDIYO NAMBA YA SIRI(PASSWORD) ILI MUNGU AKUJIBU MAOMBI YAKO.

Baada ya hapo ndipo anamwambia Musa anyoshe fimbo.Walipoendelea mbele IMANI zao ndipo bahari inagawanyika nao wanapita salama.Zaburi 126:1-2 inasema, “BWANA alipowarejeza mateka wa Sayuni,Tulikuwa kama waotao ndoto..........”.

Inawezekana kabisa umezunguka sehemu nyingi sana kutafuta suluhisho la maisha yako lakini tatizo linazidi kuwa kubwa.Yawezekana umetembea kwa waganga wengi wa kienyeji, hata kwa watumishi na makanisa mengi.Ndugu jamaa na marafiki wamekutenga.USIFE MOYO!!!! NENO ambalo Mungu amenipa kukupa siku ya leo ni kuwa ULIVYOZUNGUKA HUO MLIMA VYATOSHA.

Yawezekana umekataliwa na mchumba wako, wazazi wamekutenga, magonjwa yanakusumbua mpaka umekuwa kama muuza DUKA LA DAWA kwa wingi wa dawa uzitumiazo. Yawezekana pia mapepo na vifungo mbalimbali vinavyokutesa usiku na mchana.Huna maendeleo zaidi ya kuishi na madeni.

IMANI YAKO LAZIMA IENDELEE MBELE , USIANGALIE ULIKOPITA, TENGENEZA ULIPO NA ANGALIA MBELE. Yesu yupo kufanya kitu kwako zaidi ya ujuavyo.Mwamini Mungu na kama haujaokoka lazima uokoke ili maisha yako yapone.

NO DISEASE JESUS CANNOT CURE, NO ILLNESS JESUS CANNOT HEAL, NO PROBLEM JESUS CAN NOT SOLVE.

Kwa MAOMBI na USHAURI Au kama unataka kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako iili uone raha ya kuwa ndani ya Yesu nitafute kwa mawasiliano haya:

SIMU: 0757 350 527
EMAIL: kipangulanickson@yahoo.com
MUNGU AKUBARIKI SANA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KURUHUSU UTUKUFU (GLORY) WA BWANA KUFANYA JAMBO KATIKA MAISHA YAKO