NAMNA YA KURUHUSU UTUKUFU (GLORY) WA BWANA KUFANYA JAMBO KATIKA MAISHA YAKO



SOMO : NAMNA YA KURUHUSU UTUKUFU (GLORY) WA BWANA KUFANYA JAMBO KATIKA MAISHA YAKO

UTUKUFU(GLORY)  Udhihirisho wa utendaji kazi wa nguvu za Mungu waziwazi. EXPOSURE OF THE POWER OF GOD AT WORK

ISAYA 60;1, “ONDOKA ,uangaze; maana nuru yako imekujia na UTUKUFU WA BWANA umekuzukia.
Neno ONDOKA maana yake STEP OUT FROM………… au BE OUT OF……..

Amri ya KUONDOKA inakuja baada ya kuwa NURU YAKO PAMOJA NA UTUKUFU WA BWANA vipo tayari kwa ajili yako. Maana yake bila kuondoka mahali ulipo huwezi ukaangaza na nuru yako, lakini pia UTUKUFU WA BWANA hautaweza kutenda kazi ndani yako.

Kuondoka ni hatua ambayo inafanyika ili kujisogeza kwenye mazingira stahiki ambapo NURU yako itaangaza lakini pia UTUKUFU WA BWANA UTAKUZUKIA (utaanza kutenda kazi kusudiwa ndani yako).

Katika kitabu cha Mwanzo 12;1 – 2 Mungu anamtokea Abramu,.

“ BWANA akamwambia Abramu, TOKA/ ONDOKA wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayo kuonesha, Nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki na kulikuza jina lako nawe uwe Baraka( NGUVU).”

Hili ni agizo la Mungu kwa Abramu ambalo linamaanisha kufanyika kuwa Baraka na kuwa taifa kubwa KUNATEGEMEA IMANI pamoja na MATENDO (UTII) wa kuondoka Mahali alipo na kwenda mahali pengine ambapo pameandaliwa kwa ajili ya UTUKUFU WA BWANA KUFANYA JAMBO JUU YA MAISHA YA ABRAMU.

Suala la KUONDOKA halijalishi umependaje mazingira uliyopo au hali au marafiki ulionao. Lazima ujenge IMANI na UTII na kuchukua hatua ili kupata kilichokusudiwa.

Suala la Mungu kusema UTABARIKIWA MJINI na UTABARIKIWA MASHAMBANI halimaanishi popote tu utakapoamua kukaa utabarikiwa no no no. Lazima jambo hili liambatane na utii na kufuata maagizo yote ya Mungu anayokuagiza wakati husika. KUMBUKUMBU 28;1 – 3
NENO ONDOKA LIMEBEBA DHANA NYINGI. ZIFUATAZO NI BAADHI;

1.      Ondoka katika mtazamo, fikra,uelewa ulionao

2.      Ondoka katika KIWANGO CHA IMANI Ulichonacho

3.      Ondoka katika mazingira uliyopo

4.      Ondoka kati ya marafiki ulionao

5.      Ondoka katika desturi/mila ambazo zipo ndani ya ukoo/kabila lako

6.      Ondoka katika viwango vya utoaji ulivyonavyo

7.      Ondoka katika kiwango cha ibada ulichonacho

Isaya amekuwa nabii katika kipindi ambacho mfalme UZIA anatawala, UDUNI wake katika utumishi ni kwa sababu ya uwepo wa UZIA. Kwa tafsiri nyingine ili UTUKUFU WA BWANA UTENDE KAZI katika maisha na utumishi wa nabii Isaya, Jambo moja kati ya haya lilitakiwa litokee. Aidha ISAYA aondoke kwenye ule utawala wa mfalme UZIA au UZIA aondoke mahali alipo nabii Isaya.

ISAYA 6;1 – 8 hapa tunaona Mwaka wa kufa kwa UZIA ndio wakati Isaya nabii ANAMWONA BWANA na KUZUKIWA na UTUKUFU WA BWANA ,na ndipo anagundua kuwa katika midomo yake kuna uchafu. Ndipo Mungu anamtakasa midomo yake na uovu wake.

Cha ajabu baada ya Isaya kutakaswa ndipo Mungu anauliza nimtume nani. Lakini kumbuka katika sura tano zilizopita Isaya anatumika na Bwana na kuoneshwa maono mbalimbali.

Jambo la kujifunza hapa ni kuwa:-
1.       
     Wakati mwingine utukufu wa Mungu haujidhihirishi katika maisha yako kwa sababu tu ya uwepo wa mtu au watu Fulani uliowabeba moyoni mwakoau katika maisha yako. Yawezekana wakawa ni marafiki, jamaa, ndugu, familia, viongozi n.k , ndiyo sababu ya Mungu kumwambia Abramu aondoke kati yao.

2.      Dhambi ni jambo ambalo hukufanya NURU yako kutokuangaza na kufanya UTUKUFU WA MUNGU  usitende kazi ndani ya maisha yako.

3.      Kuna kiwango Fulani cha wito hakiwezi kuachiliwa kwako na Mungu kutokana na kutoondoka katika mazingira, watu au dhambi Fulani.

a.       Uchafu wa Isaya ulikuwa tu katika kunena lakini ilimzuia kutoitwa na Mungu kwa kiwango cha juu mpaka pale alipo takaswa ndipo Mungu akasema nimtume nani? Bado anatafuta utayari ndani ya Isaya wa kukubali kuondoka katika hali yake hiyo.

UTUKUFU WA BWANA unaposhuka mahali unatatua matatizo ya watu kwa namna ya kujitegemea. Maana yake kama ni kuponya, kufungua, kuinua, kuhuisha n.k unaachilia juu ya watu waliopo katika eneo hilo.

2Nyakati 5;13 – 14.
Hapa tunaona utukufu wa Bwana kwa mfano wa wingu uliposhuka anasema hata makuhani hawakuweza kufanya huduma yao kwa sababu ya UTUKUFU WA BWANA.

MAANA YAKE utukufu wa BWANA unapokuwepo mahali unaponya wenyewe, unafungua wenyewe, unahuisha na kurejesha wenyewe. Hata hakuna haja ya makuhani/watumishi kuita watu kuokoka mara mbili mbili, wao wenyewe wanajipeleka mbele tena kwa mguso na kulia, huku wakijutia dhambi zao kwa kumaanisha.

UTUKUFU WA MUNGU ni ishara ya kuwepo kwa UFALME WA MUNGU MAHALI na kumbuka ufalme wa Mungu unapokuwepo mahali LAZIMA mapenzi ya Mungu yatatimizwa Duniani kama Mbinguni (ulimwengu war oho). RUDIA KUSOMA HII SENTENSI kuna kitu utapata zaidi hapa.

Luka 2;8 – 11 (utukufu ulishuka kwa kuwa Yesu Mfalme amezaliwa eneo lile)

Mathayo 6; 9 – 10 (ufalme wa Mungu unapokuwepo mahali mapenzi ya Mungu au mipango ya Mungu juu ya hapo mahali au watu fulani iliyopangwa mbinguni inadhihiriika kiuhalisia)

MWAMBIE MUNGU NINATAMANI KUUONA UTUKUFU WAKO UKITENDA JAMBO KWEYE MAISHA YANGU KATIKA JINA YA YESU



UHUSIANO WA UTUKUFU WA BWANA NA UTAKATIFU WA MAHALI UNAPOSHUKA

Kujifunua kwa utukufu wa Mungu kunategemea na hali ya utakatifu iliyopo mahali au ndani ya mtu.

Waebrania 12;14, “ Tafuteni kwa BIDII kuwa na amani na watu wote NA HUO utakatifu AMBAO hapana mtu ATAKAYEMWONA MUNGU( UTUKUFU WAKE/MATENDO YAKE) asipo kuwa nao.”

Suala la kumwona Mungu hapa halizungumzii tu katika siku ya mwisho,, maana siku ya mwisho kila jicho litamwona hata hao waliomchoma (UFUNUO 1;7 ).  Hapa ana maana ya kuwa UTAKATIFU pekee ndio ambao unakufanya umwone Mungu katika maisha yako, ndoa yako, biashara zako, elimu yako n.k.

Kuna msemo huwa nawaambia watu ninapoomba nao kuwa Mungu wetu sio mganga wa kienyeji. Maana yangu hapa ni kubwa sana. Ninamaanisha kuwa wapo watu wengi ambao wanataka sana Mungu AWAGUSE katika shida zao lakini wao wenyewe hawataki KUMGUSA Mungu kwa matendo yao mema na Uchaji. Uovu wako na dhambi zako zinauzuia UTUKUFU WA BWANA kukuzukia na laiti ungejua hilo usingekalia kulaumu kuwa kwanini nimeokoka, ama sioni umuhimu wa kwenda ibadani. Ungelia na kumrudia Mungu kwa kuombolea na kuugulia moyo na Mungu angejitokeza kwako mara. ISAYA 59;1 – 2 .

Katika kitabu cha KUTOKA SURA YA 3, Musa anapoambiwa avue viatu vyake maana mahali pale ni patakatifu, maana yake bila Musa kuvua viatu hawezi akaona udhihirisho wa utendaji kazi wa Mungu waziwazi yaani UTUKUFU WA MUNGU. Ndio maana baada ya kuvua viatu anaanza kuona ishara na maajabu ya Mungu kwake mwenyewe na sio kwa kusimuliwa. Na anapata fursa ya kumjua Mungu kwa jina (NIKO AMBAYE NIKO). La sivyo angeishia kuona tu kijiti kinachowaka bila kuteketea na maisha yake yanabaki kuwa duni mpaka wa leo.

 Usipokubali kuishi katika utakatifu na uchaji (kuvua viatu)  utaishia kushuhudia wengine wakikombolewa na kuwekwa huru, kuinuliwa na kuponywa lakini wewe unabaki kuwa duni. Suala sio kuwa kanisani kwenu kuna miujiza na ishara nyingi , hapana., cha msingi hiyo miujiza na ishara vinakusaidiaje kwenye maisha yako kiroho na kimwili??? Je, kuna namna unasogea katika mafanikio au unashuhudia tu wengine wakisema,, Nmshukuru Mungu sasa nimepata kazi, mchumba, mtoto, chuo, nk. Kaa katika utakatifu maana pasipo huo hauwezi KUMWONA BWANA( KI UTUKUFU) usipokuwa nao.

Biblia inasema TAFUTENI KWA BIDII. UTAKATIFU unatafutwa kwa bidii. Lazima ufunge, na kulia kwa toba na unyenyekevu siku kwa siku. Makwazo hayana budi kuja kwako lakini je, unayabebaje? Mara nyingi umekalia kujihesabia haki na kuwalaumu ama kuwashutumu wengine juu ya hali uliyonayo lakini umesahau kuwa Mungu anapofungua milango kwa ajili yako Hakuna awezaye kufunga ISIPOKUWA wewe mwenyewe? (UFUNUO 3;7 – 8 ) .Hakuna mtu amekufungia kazi yako, mke/mume wako, watoto wako ama biashara yako. Ni wewe mwenyewe maana ukisimama imara hakuna milango iliyofunguliwa na Mungu ambayo itafungwa na shetani, wachawi, maadui, waganga wa kienyeji, mizimu, n.k.  Kiini cha Shida yako ni wewe kutokaa vema na kujua  step /HATUA za jinsi gani uenende katika Bwana kwa wito ulioitiwa. ( WAEFESO 4; 1 – 3 ).

Wokovu nao ni wito ambao mwanadamu unaitwa na Yesu na lazima kunakuwa na hatua za kuzifuata ili ufikishwe mahali ambapo huyo aliyekuita amekuandalia. Wapo watu wengi wanakiri kuokoka na wanakiri kupenda wokovu LAKINI sio wengi wanapenda na kufuata HATUA ZA WOKOVU kuwapeleka mahali ambapo Bwana Yesu amewaandalia kwa maisha ya hapa duniani na Mbinguni pia. (MARKO 10; 28 – 31 )

Utakuta mdada anasema ameokoka lakini mtoko wake ni  VIMINI SKETI, VIJISURUALI, VITOP, MATITI NJE, MIKOROGO, LUGHA CHAFU, KUBADILISHA WANAUME KILA SIKU HATA WAUME ZA WATU N.K. hapo dadaangu ni ngumu sana kumwona Mungu akifanya kazi kwako hata kama unafunga siku saba kavu au hata kama unasali kwenye ngurumo ya upako, Mlima wa Moto n.k

AU utakuta mkaka anasema ameokoka na ni mtumishi lakini mitoko yake ni VIJISURUALI VYA KIKE, MACHENI MAKUBWA, MILEGEZO/KATA K, HELENI, MAPETE PETE YASIYOELEWEKA NI YA NDOA AMA UCHUMBA, LUGHA CHAFU, KUTEMBEA NA WAKE ZA WATU NA VISICHANA N.K hapo my RESPECTIFUL BROTHER unajilisha upepo, ni ngumu sana kuuona utukufu wa Mungu hapo aisee.

Mungu wetu kama alivyo mtakatifu nasi imetupasa kuwa watakatifu ( 1PETRO1;16 – 19 ). Utakatifu ni sifa ya mtu aliyeokoka na siyo majivuno Fulani .  UTAKATIFUunaletwa na kutakaswa kwa damu ya Yesu kila iitwapo leo. UFUNUO 22;11.,12;11.

Utukufu wa Bwana unapoondoka Adui wanapata nguvu dhidi yako. Lazima kuutunza utukufu wa Bwana kama vile wana wa Israeli na SANDUKU LA AGANO.

Tusome 1 SAMWELI 4;19 – 22 ,Tena mkwewe, mkewe huyo Finehasi, alikuwa mja-mzito, karibu na kuzaa; basi, aliposikia habari ya kutwaliwa sanduku la Mungu, na ya kwamba mkwewe na mumewe wamekufa, akajiinamisha, akazaa; maana utungu wake ulimfikilia.Hata alipokuwa katika kufa, wale wanawake waliohudhuria karibu naye wakamwambia, Usiogope; kwa maana umezaa mtoto mwanamume. Walakini hakujibu, wala hakumtazama. Akamwita mtoto, Ikabodi, akisema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; kwa sababu sanduku la Mungu lilikuwa limetwaliwa, na kwa sababu ya mkwewe na mumewe.Naam, akasema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; maana sanduku la Mungu limetwaliwa.

TUONE KIDOGO HAPA KWA HABARI YA SANDUKU LA AGANO

Hili ni sanduku la Agano ambalo ndani yake kulikuwa na Mbao mbili za mawe zilizobeba Amri kumi. Pia kulikuwa na fimbo Ya Haruni ambayo ni Ishara ya Mamlaka kadhalika kulikuwa na kopo la dhahabu lenye mana. EBRANIA 9;4. Ndilo lililobeba utukufu wa Bwana yaani Udhihirisho wa nguvu za Mungu. Ndio maana unakuta kila mahali ambapo wana wa Israeli wanakuwa nalo wakiwa katika utakatifu, linafanya makuu. Kipindi cha Yoshua lilifanya Mto Yordani ufunguke na kuachia njia.

Sanduku la Agano la Sasa ni MOYO WAKO. Ndani yake lazima kuwe na Mbao Mbili za mawe yaani Amri za Mungu na sheria zake

2WAKORINTHO 3;2 – 3 , “Ninyi ndinyi barua yetu, iliyoandikwa mioyoni mwetu, inajulikana na kusomwa na watu wote; mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo tuliyoikatibu, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama.

Lazima pia kuwe na Kopo la Mana, maana yake chakula cha uzima au Neno la Mungu. YOHANA 6;31 – 35 .

Pia lazima kuwe na Fimbo ya Haruni yaani mamlaka au Jina la Yesu na mamlaka yake.(Luka 10;19)

Sanduku la Bwana ndio utukufu wa Bwana. Utukufu wa Bwana unapokuwepo unaachilia Mbinu na UFUNUO juu ya jambo Fulani.  Bila utukufu wa Bwana ndani yako kunaitwa IKABODI maana yake utukufu wa Mungu umeondoka.

UFUNUO USIPOKUWEPO mhubiri anaishiwa mahubiri, anabakia kuhubiri kwa KALENDA na LITRUGIA.  Mwimbaji anaishiwa nyimbo, anaanza kuiga nyimbo za watu wa dunia (warumi 12;2) na wakati Mungu anasema mwimbieni Bwana wimbo Mpya maana yake unaokuja kimafunuo. ZABURI 96;1-3. Mwombaji unaishiwa maombi, unabaki kuomba kwa matukio yaani kwa sababu unajua Fulani anasafiri unakemea roho za ajali, au kwa sababu Fulani anaumwa unakemea roho za mauti, lakini hakuna ufunuo wowote utakuwa unaupata na ndio maana unakaukiwa maombi.

Ipo tofauti kati ya KNOWLEDGE (MAARIFA) na REVELATION (UFUNUO)

MAARIFA[KNOWLEDGE] ni kujua maelezo ya kitu Fulani kilivyo. Hii hata mtu ambaye hajaokoka anaweza kuwa nayo. Ndio maana watu wengi wanaofundisha bible knowledge au wanaosoma elimu ya biblia unakuta wengine hawajaokoka kabisa.

UFUNUO [REVERATION] ni kuwekwa wazi kwa hali au jambo Fulani linaloendelea kwa namna ya rohoni au namna jambo lilivyo kwa namna ya rohoni. Hii ni kazi ya Roho Mtakatifu pekee. Ndiyo maana mtu anayefunuliwa lazima awe ameokoka maana yake anaishi maisha matakatifu.

Maarifa yanazuia usiangamie LAKINI mafunuo yanafanya ufanikiwe na kuinuliwa viwango na wakati mwingine kukufanya ujue kiini cha tatizo lilivyo na namna ya kulitatua.

Ndani ya NENO kuna utukufu wa Mungu na ili uuone huo utukufu wa Mungu ndani ya NENO lazima NENO afanyike mwili yaani adhihirike kiuhalisia ndani yako na KUKAA NDANI YAKO (YOHANA 1;14).Na utukufu wa Mungu ukionekana unaachilia NEEMA na KWELI inayokufanya uwe huru (YOHANA 8;32)  na umshinde/uvunje kazi za Ibilisi. (1 YOHANA 3;8B)

MAMBO YA KUZINGATIA
1.      TUNZA UTAKATIFU NA KUUTAFUTA KWA BIDII – WEBRANIA 12;14
2.      SHIKA NENO NA LIKAE NDANI YAKO – YOHANA 1;14, WAKOLOSAI 3;16
3.      NYENYEKEA KWA BWANA – 1PETRO 5; 6 – 7
4.      KAA MAGOTINI/ UWE MWOMBAJI – WAFILIP 4;6
5.      IMBA SIFA ZA BWANA HATA KATIKA MAGUMU – 2 NYAKATI 5; 13 – 14
6.      TUNZA HEKALU LA MUNGU/ MWILI WAKO – 1 WAKORINTHO 3;16 – 17
7.      ONDOKA/ JITENGE NA MAMBO YAKWAMISHAYO – ISAYA 60;1 – 3
8.      ITIKA WITO KWA BWANA/ KUBALI KUTUMIKA – ISAYA 6;8, YOHANA 12; 26

Mungu Akubariki Sana Kwa Kulipata Somo Hili.

AMBATANA nami katika SALA HII kwa IMANI

MUNGU WANGU, BABA YANGU, ASANTE KWA UPENDO WAKO WA THAMANI,
NISAFISHE UOVU WANGU NA DHAMBI ZANGU KWA DAMU YA YESU,
NIWEZESHE KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU,
IFANYE NURU/ NYOTA YANGU IANGAZE NA UTUKUFU WAKO UKANIZUKIE KATIKA MAISHA YANGU NA UKAFANYE JAMBO NDANI YA MAISHA YANGU,
FUNGUA MILANGO ILIYOFUNGWA MBELE YANGU NA NIFANYE KUPIGA HATUA KUKUELEKEA WEWE,
NIKAFANIKIWE DUNIANI KATIKA MAMBO YOTE  NA HATA UZIMA WA MILELE ,
KATIKA JINA LA YESU!! AMEEEN.

KWA USHAURI,MAOMBI NA MAOMBEZI AU KUSHIRIKI BARAKA HIZI KWA NJIA YA SADAKA,

TUTAFUTE KWA:
SIMU: 0757 35 05 27( SMS &WATSAPP) AU 0717 23 64 90 (SMS)
EMAIL; nicksonkp@gmail.com
BLOG; www.urejesho.blogspot.com
Imeandaliwa na ;mwl .NICKSON KIPANGULA WA HUDUMA YA MAOMBI YA UREJESHO

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog