NAMNA YA KURUHUSU UTUKUFU (GLORY) WA BWANA KUFANYA JAMBO KATIKA MAISHA YAKO
SOMO : NAMNA YA KURUHUSU UTUKUFU (GLORY) WA BWANA KUFANYA JAMBO KATIKA MAISHA YAKO UTUKUFU(GLORY) – Udhihirisho wa utendaji kazi wa nguvu za Mungu waziwazi. EXPOSURE OF THE POWER OF GOD AT WORK ISAYA 60;1, “ONDOKA ,uangaze; maana nuru yako imekujia na UTUKUFU WA BWANA umekuzukia. Neno ONDOKA maana yake STEP OUT FROM………… au BE OUT OF…….. Amri ya KUONDOKA inakuja baada ya kuwa NURU YAKO PAMOJA NA UTUKUFU WA BWANA vipo tayari kwa ajili yako. Maana yake bila kuondoka mahali ulipo huwezi ukaangaza na nuru yako, lakini pia UTUKUFU WA BWANA hautaweza kutenda kazi ndani yako. Kuondoka ni hatua ambayo inafanyika ili kujisogeza kwenye mazingira stahiki ambapo NURU yako itaangaza lakini pia UTUKUFU WA BWANA UTAKUZUKIA (utaanza kutenda kazi kusudiwa ndani yako). Katika kitabu cha Mwanzo 12;1 – 2 Mungu anamtokea Abramu,. “ BWANA akamwambia Abramu, TOKA/ ONDOKA wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayo kuonesha, Nami nita