UWEZO
WA KUTAWALA
NA
KUMILIKI
ARDHI/NCHI
KWA
NJIA
YA
MAOMBI
NA MWL. NICKSON KIPANGULA
MFUMO
WA KIROHO UNAOTOA KIBALI CHA KIFALME
Dhana ya ufalme imeanzia
katika kitabu cha MWANZO 1; 28
Inasema, “ Mungu akawabarikia
(akaachilia NGUVU) , Mungu akawaambia, zaeni (be fruitful), mkaongezeke(
multiply), mkaijaze nchi na KUITIISHA; MKATAWALE samaki wa baharini, na ndege
wa angani, NA KILA kiumbe CHENYE UHAI kiendacho juu ya nchi (LAND).”.
Vipo vitu vya kujifunza
hapa;
1.
Kumbe lengo kuu la Mungu kumuumba mtu ni
kuwa aweze kutawala na kutiisha NCHI pamoja na kila kiumbe ili mradi kipo ndani
ya nchi.
Ø KUMBUKA
mtu ni roho, anayo nafsi , na anaishi ndani ya mwili. MAANA YAKE hayo maagizo
yote anaachilia kwa roho ambayo baadaye ataiumbia mwili .
2.
Pia anaposema, AKAWABARIKIA maana yake
AKAACHILIA NGUVU ya kufanya kile ambacho anawapa kukifanya ambacho ni KUTAWALA
na KUTIISHA.
Ø Maana yake bila NGUVU huwezi kutawala na
kutiisha chochote.
3.
KUTAWALA NA KUTIISHA hii ni dhana ya
ufalme.
Ø KUMBUKA
kiongozi yeyote anaweza kutawala kwa maana ya kuongoza lakini MFALME pekee
ndiye anaweza kutiisha KWA MAMLAKA aliyonayo.
4.
Suala la kuzaa halipo tu katika dhana ya
watoto kwenye biblia za kiingereza imeandikwa, BE FRUITFUL. MAANA YAKE zaeni
matunda.
Ø Kwa
tafsiri nyingine ni kwamba ndani ya mtu ameweka MBEGU(SEEDS) na kuachilia nguvu
(BARAKA) ya kuzaa au kutoa matunda sawasawa na Mbegu ambayo ameweka.
5.
Kumbe kila kiumbe chenye uhai kinatawaliwa na kutiishwa na mtu.
Ø Na
sio tu chenye uhai ili mradi kinaunda nchi (land) kimepewa mtu awe mtawala na
mtiishaji wake. Mfano bahari, mito, mawe, milima, upepo, mvua, jua, N.K
6.
KUTAWALA na KUTIISHA kupo katika
ulimwengu wa roho maana yake kunatumia MFUMO WA KIROHO WA KIUTAWALA na ndiyo
maana anawasemesha Adamu na hawa kabla ya kuumba miili yao, punde tu baada ya
kuumba roho zao.
UFALME ni milki/mali ya
mfalme, eneo ambalo lina mipaka kamili (territory) na lina mfumo Fulani wa
kwake kiuchumi, kiutamaduni na kimila pamoja na Ibada. Ndani ya ufalme kuna watu ambao wanatawaliwa
na mfalme ambao inawezekana ni raia (citizen) ama watumwa.
MFALME
ni Yule ambaye ufalme upo chini yake maana yake anayemiliki huo ufalme, watu na
kila kilichomo ndani ya huo ufalme.
Ukiisha
itwa ufalme lazima kuna mfalme. Ukipewa ufalme maana yake wewe ni mfalme katika
eneo hilo.
LUKA
12;32, “Msiogope enyi kundi dogo, kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule
UFALME”. Kwa tafsiri nyingine anasema
kwa kuwa baba yenu ameona vema kuwapa ninyi kuwa wafalme katika eneo hilo la ufalme.
Mfalme
hatawali kwa kutumia mawazo ya wengi, mijadala,ama mapendekezo ya raia wake ama
viongozi wengine wafanyavyo. MFALME anatawala kwa KUTUMIA NENO/AMRI.
Wakati
Yesu amepigiliwa misumari msalabani PILATO aliweka kibao juu ya Msalaba
kisemacho, “YESU MNAZARETI, MFALME WA
WAYAHUDI”. Wapo watu walipinga na kushauri kibao kitolewe lakini Pilato kwa
Mamlaka ya Kifalme akawaambia “NILIYOANDIKWA NIMEYAAANDIKA”. ( YOHANA 19;19 –
22 ). Hiyo ni Amri/neno la kifalme, na
tunaona hakuna mtu aliyeendelea tena
kubisha bisha.
Mungu
anatawala kifalme ndiyo maana hata katika uumbaji tunaona anaamuru kwa kusema
IWE NURU – INAKUWA ,NA LIWE ANGA KATIKATI YA MAJI… - LINAKUWA, NCHI IZAE KIUMBE
HAI… - INAZAA N.K. huu ndio mfumo wa
kifalme. Unatumia NENO na AMRI siyo ombi na hakuna namna NURU itasema ooh
subiri kwanza… au sitaki… n.k.
MHUBIRI
8;4, “ kwa kuwa NENO LA MFALME lina NGUVU, naye ni nani awezaye kumwambia huyo
wafanya nini?”
Mfalme
akiisha kuongea maana yake ametoa maamuzi ya mwisho ambayo hayawezi kuhojiwa na
yeyote wala kujadiliwa kwa dhana ya kupinga. Ndiyo maana KWA MUNGU tu kuwa
mfalme kunaondoa dhana ya kujadili au kurekebisha NENO LOLOTE ambalo amelisema
kwa kinywa chake. Hata kama kwako halikupendezi ama unaona gumu kulifuata.
Mfumo
wa kiutawala ambao Mungu ameuweka asili ni kwamba YEYE ATAWALE MBINGUNI NA
DUNIANI na mwanadamu atawale DUNIANI. Maana yake Mungu amekusudia atawale
duniani kupitia mwanadamu aliyemuumba na kuweka kwa kutumia neno/amri ya Mungu.
UUNGU
ni UFALME ndiyo maana baada ya mwanadamu kumkabidhi shetani nafasi ile, shetani
akaitwa mungu wa dunia hii. Nafasi ambayo alikuwa nayo mwanadamu kabla ya
kuasi.
Soma
ZABURI 82; 6, “ Mimi nimesema , ndinyi miungu, Na wana wa ALIYE JUU , nyote
pia”.
Pia
katika ZABURI 115;15-16, “Na mbarikiwe (MPEWE NGUVU) ninyi na BWANA,
aliyezifanya mbingu na nchi. MBINGU NI MBINGU ZA BWANA bali nchi AMEWAPA
WANADAMU.”
MAANA
YAKE Mungu ndiye aliyeifanya mbingu na nchi lakini kwa namna ya utawala ameamua
amkabidhi mwanadamu kama mfalme aisimamie, aitawale na kuitiisha. Ndiyo maana
yeye anaitwa mfalme wa wafalme, maana yake wewe ni mfalme lakini yeye ndiye
mkuu wako. NDIYO MAANA UNATAWALA KIMAMLAKA KWA KUTUMIA NENO LAKE na siyo NENO
LAKO.
Baada
ya mwanadamu kuupoteza ufalme aliopewa na kumkabidhi shetani kwa sababu ya
udhaifu, Mungu akaandaa Mfumo mpya wenye nguvu wa kumuuingiza mwanadamu katika
UFALME JUU YA DUNIA kwa namna ya kiroho tena.
UFUNUO
5;9-10, “ Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewekukitwaa hicho kitabu
na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa (kusulibishwa au kufanyika
sadaka ya kuteketezwa), ukamnunulia Mungu kwa Damu yako watu wa KILA kabila,na
lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa UFALME na MAKUHANI kwa Mungu wetu; nao
WANAMILIKI JUU YA NCHI”. Sema tena …”NAO WANAMILIKI JUU YA NCHI..”
Kumbuka
nimekuambia kuwa ANAYEMILIKI NI MFALME PEKEE.
Na
mfumo ambao Mungu ameuweka wa mwanadamu kumiliki juu ya nchi ni kwa njia ya
UFALME NA UKUHANI.
Inawezekana
unajiuliza kwa NINI UKUHANI UKAINGIA HAPO????. SIKILIZA; UMILIKI ambao Mungu
ametupa ni kwa njia au namna ya Kiroho. UKUHANI unafanya kazi ya utakaso au toba ili
kuweza kuunganisha MBINGU na NCHI/ARDHI ya eneo lolote ambalo umepewa kumiliki.
NDIYO
MAANA unabaki kusema, nimeambiwa kila nitakapokanyaga nimepewa kumiliki mbona
ninateswa na nchi na vilivyomo?? Mbona ardhi inanizalia miiba na michongoma????
Mbona wachawi wananimiliki??? SUALA hapa sio kukanyaga suala hapa ni je,
UNAKANYAGAJE???. LAZIMA ukanyage mkanyago wa KIKUHANI kwanza, yaani toba juu ya
ardhi hiyo na BAADAYE mkanyago wa KIFALME kusema neno la kifalme kwa kutumia
NENO LA MUNGU juu ya huo ufalme au nchi/ ardhi unayotaka umiliki na kutiisha.
Danieli
Mbali na kuwa ni mtoto wa Mungu alijikuta katika wakati mgumu ambapo maombi
yake anayoomba hayana majibu, ni mpaka alipoingia kwenye maombi ya siku 21 ya kuunganisha Mbingu na ardhi aliyopo.
KUMBUKA Wakati huo Danieli yupo utumwani maana yake siyo katika ardhi
anayoijua.Kwa maana hiyo yupo kwenye ardhi ya uovu maana inamilikiwa na utawala
wa mataifa wasiomjua Mungu. DANIEL 10;1-13.
Fahamu
Ardhi ya eneo inapomilikiwa na adui kunakuwa na kukatika kwa mawasiliano (
TOTAL DISCONNECTION) kati Ya Mbingu na ARDHI/ NCHI. Muunganiko wa Baraka za
Mungu au majibu ya kimungu kukufikia unakuwa ni mgumu sana kwa maana MKUU WA
ANGA(PEPO) anatawala kutokana na kibali kutoka hapa chini ardhini/nchi na siyo
kwamba anapata kuzimu no, no ,no. maana
yake kukiwepo na mfalme ambaye ni wa kuzimu, Mkuu wa anga atatawala na kukiwepo
na mfalme ambaye ni wewe katika hilo eneo maana yake anga lake litakuwa na
Malaika.
Madhara ya mkuu wa anga kutawala anga ni kuwa
anakuwa na uwezo wa kuzuia kila jambo jema linaloachiliwa kutoka mbinguni na
pia anakuwa na uwezo wa kuachilia mabaya juu ya nchi kwa kushirikiana na
mawakala wengine wa shetani. Vile vile, Wachawi, mapepo, majini, waganga wa
kienyeji, mizimu n.k vinapata uhalali wa kutawala eneo na watu wa eneo na
kulitumia kwa kupata KIBALI kutoka kwa mkuu wa anga la eneo lile ambaye naye
anapata fursa ya kutawala kutoka kwa mfalme aliyepo katika ardhi/nchi hiyo
husika.
Kilichomfanya
Yesu akubali Kutoyatoa mapepo ya mtu wa nchi ya Ugerasi nje ya mji siyo kwa kuwa
Yesu anayatii mapepo la hasha,, ni kutokana na SHERIA YA UFALME, maana yake wao
walikuwa na uhalali wa kumiliki lile eneo ndiyo maana wakasema hata kama
ukitutoa kwa huyu mtu tunaomba usitutupe shimoni (usitutoe mipakani mwa hii
nchi) afadhali turuhusu tuwaingie nguruwe wale, na kwa kuwa wapo kwenye miliki
yao akawaruhusu.
Na
ndiyo maana utakuta kwamba Yesu baada ya kumfungua mtu Yule hakukubali Yule mtu
afuatane naye kwa kuwa anataka ampe kazi katika nchi/ardhi yake ya kumiliki,
kutiisha na kuondosha ufalme wa giza katika nchi/ ardhi yote ya Ugerasi.
Tusome
LUKA 8;37-39, “ Na jamii ya watu wa nchi/ ardhi ya Wagerasi iliyo kando kando
walimwomba (YESU) aondoke kwao, kwa kuwa walishikwa na hofu nyingi……[ yawezekana
wakajua kaja huyu sasa mifugo yetu kwisha habari yake,,, maana yale mapepo ni
mwendo wa kuzunguka mara kwa nguruwe, mara itakuja kwa ng’ombe baadaye kwa
mazao ya shamba n.k ili mradi tu yana uhalali wa kukaa katika nchi ile]. Na mtu
Yule aliyetokwa na pepo alimwomba ruhusa afuatane naye; lakini yeye alimwaga
akasema, Rudi nyumbani kwako UKAHUBIRI yalivyo makuu Mungu aliyokutendea.
Akaenda zake, akihubiri KATIKA MJI WOTE,
yalivyo makuu mambo aliyotendewa na Yesu”.
NAMNA
AMBAVYO NGUVU ZA MUNGU NDANI YAKO ZINAVYOKUSAIDIA KUTIISHA KILA KITU KATIKA
NCHI/ARDHI
Katika sehemu ya kwanza
tumeona kidogo maana na tafsiri ya UFALME NA FALME, na mwanzo wa ufalme wa
Mungu aliompa mwanadamu na alivyoupoteza na kuukabidhi kwa shetani, hatimaye
Yesu kuurejesha tena.
Pia tukaona kidogo juu
ya uhusiano wa Ardhi na Mbingu pamoja na Anga. Sasa ,tusogee kidogo;
Tukisoma Efeso 3;20
inasema, “ Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya MAMBO YA AJABU MNO kuliko YOTE tuyaombayo
au tuyawazayo, KWA KADIRI ya NGUVU
itendayo kazi NDANI YETU;”
Hapa anachokisisitiza
mtume Paulo ni hiki; Utendekaji wa mambo ya ajabu mno haufanyiki kwa kutegemea
kiwango gani cha maombi unafanya ama kiwango gani cha IMANI(…TUYAWAZAYO…)
ulichonacho la hasha. UTENDAJI WA MAMBO YA AJABU MNO unategemea na KIWANGO CHA
NGUVU YA MUNGU KILICHOMO NDANI YAKO.
Ndiyo maana tuliona
katika kitabu cha Mwanzo kuwa BARAKA maana yake NGUVU na anaposema Mungu
akawabarikia maana yake Mungu akaachilia nguvu ambazo zitawapa kiwango cha
uwezo wa kutawala na kutiisha nchi na vilivyomo.
Hii ndiyo siri
iliyomfanya Yesu awe anashinda muda mwingi mlimani akimwomba Mungu. Watumishi
wengi huomba kwa mzigo pale tu wanapokuwa na huduma, semina ama mkutano wa
injili. Matokeo yake anajikuta anaishiwa nguvu mapema. Yesu haikujalisha mchana
atakuwa na huduma ama hana huduma, jioni lazima apitie mlimani kuomba. Na cha
ajabu ni kuwa hakuna mwanafunzi
anamwambia Yesu leo twende pamoja basi!!!!.
Wanamshangaa tu kuwa
duh, hata upepo na mawimbi ya bahari vinamtii?? Suala halikuwa kwamba IMANI tu
la hasha, SUALA NI ILE NGUVU YA MUNGU NDANI YAKE inayokusanywa kwa njia ya
maombi ndiyo ilimfanya atembee juu ya bahari, afufue wafu, aponye vipofu,viwete
n.k.
Kutembea juu ya maji ,
kufufua wafu, kuponya wagonjwa, kutoa pepo kwake Yesu halikuwa ni jambo la ajabu
wala kuita muujiza la hasha, Yalikuwa ni maisha yake ya kawaida sana ya kila
siku kwa kuwa alijua kutafuta na hatimaye kutumia nguvu ya Mungu iliyomo ndani
yake kutawala na kutiisha nchi na kila kilichomo.
Mfumo ambao Mungu
ameuandaa kwa namna ya kimawasiliano kati yako na ulimwengu wa roho ni maombi. Maombi ndiyo yanayoachilia Nguvu
za Mungu kukuwezesha kutawala na kutiisha.
KWA MUNGU – unafanya maombi,,,,, KWENYE VITU – unaachilia nguvu ili kifanyike chochote
unachotaka kifanyike. Maadamu Kiwe ndani ya Mamlaka ya Neno la Mungu (maana
yake NENO LA MUNGU liwe limejieleza kuwa na uwezo/UHALALI wa kufanya hicho
kitu).
PASIPO MIMI, NINYI
HAMWEZI NENO LOLOTE,, YOHANA 15;4-5.. Maana yake USIPO KUWA na Nguvu za Mungu
ndani yako kupitia Maombi ningumu sana kuuendesha utawala waadui katika ardhi
au eneo ulilopo.
ISAYA 37;3 – 4, “
Wakamwambia, Hezekia asema hivi, Siku hii ni siku ya dhiki, na aibu na
matukano; maana watoto wa tayari kuzaliwa, wala hapana NGUVU ya kuwazaa.
Yamkini BWANA , Mungu wako, atayasikia maneno ya huyo amiri ambaye mfalme wa
Ashuru, bwana wake, amemtuma ili amtukane Mungu aliye hai; na BWANA, Mungu wako
atayakemea maneno aliyoyasikia; basi inua DUA yako kwa ajili ya mabaki
yaliyobakia.”
Mfalme Hezekia amepewa
milki ya eneo la Yerusalemu kwa Namna ya kiroho na Kimwili. Inafika mahali
anakuta maadui wanawapiga na kuwararua na mbaya zaidi anashangaa mpaka Amiri wa
Mfalme wa Ashuru anathubutu kumtukana Mungu Lakini Mungu yupo kimya. Amesahau
kuwa Mungu anatawala dunia kupitia mwanadamu na Shetani anatawala dunia kupitia
mwanadamu.
HAKUNA ROHO YOYOTE ITAKUWA NA UHALALI WA
KUTAWALA AU KUFANYA OPERATION YOYOTE KATIKA DUNIA BILA KUPITIA MWANADAMU.
Na ndiyo maana Hata shetani alipotaka
kupata umiliki halali wa dunia alimtumia Mwanadamu katika bustani ya Edeni. Vile
vile baada ya kuona Yesu amefanikiwa kupewa mwili ili apate uhalali wa kutawala
na kumiliki Dunia na hatimaye amkabidhi huo ufunguo wa utawala na umiliki
mwanadamu ( kanisa) , alijaribu kumlaghai Yesu mapema Kuwa ukinisujudia nitakupa
vyote ili amwangushe mkenge akashindwa na ndiyo maana hatimaye Yesu
akamnyang’anya ufunguo wa MAUTI na kuzimu na kulikabidhi kanisa ( MATHAYO 16;18
-19 ) na akaandaa sheria (WARUMI 8;1 -2
).
Sasa huyu Mfalme
Hezekia anapogundua kuwa Mungu hawezi ingilia kati vita hiyo hata kama
anatukanwa na watu wake wanaangamia. Lazima atumie mtu Fulani ili ajipatie
uhalali wa kuporomosha mashambulizi kwa Mfalme wa Ashuru. Anamwomba Isaya ainue
dua kwa Mungu ili kuachilia NGUVU za kuwazaa watoto (USHINDI DHIDI YA ASHURU)
na kwa ajili ya mabaki yaliyosalia.
Kumbuka hawa ni Israeli
taifa la Mungu lakini wanajikuta ardhi yao imetekwa na Mfalme wa Ashuru na
kwenye maono, ndoto, n.k wanaona kabisa ni milki yao kwao lakini katika
uhalisia au uliwengu wa mwili wanajikuta bado wapo chini ya milki ya adui.
Katika Isaya 40;30-31,
“ Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume
vijana WATAANGUKA, bali WAMNGOJEAO ( WAMWOMBAO/WAMTAFUTAO) BWANA
watapata NGUVU MPYA; Watapanda Juu Kwa Mbawa Kama Tai; Watapiga Mbio, Wala
Hawatachoka; Watakwenda KWA MIGUU Wala Hawatazimia.”
·
Kinachofanya vijana wazimie ni kukosa
NGUVU ( YA MUNGU) ya kiwango Fulani ambayo ingewafanya wakabiliane na mazingira
mapya wanayokutana nayo.
·
Wamngojeao BWANA watapata NGUVU MPYA. Maana yake katika kila
hatua au jambo lolote linalowakabilii wanapata NGUVU INAYOZIDI mazingira hayo
kiasi kwamba wanapata uwezo wa kumiliki na kutiisha KILA mazingira yaliyopo mbele yao.
KURUKA JUU KAMA TAI
MAANA YAKE:-
1.
Kuwa juu ya uwezo wa adui na hivyo
kufanya urahisi wa kupambana naye
2.
Kupata fursa ya KUONA kila
kinachoendelea chini ya ardhi na kujua hazina zako zilizofichika katika Ardhi
kwa namna ya kiroho. NDIYO SABABU anasema utapata NGUVU MPYA maana yake siyo kama ile ya nyuma katika ukuu wake.
Yesu alipowatuma
wanafunzi kuhubiri tunaambiwa WALITOA PEPO mpaka wakaja kumsimulia Yesu. Lakini
kuna siku nyingine Yesu amepanda mlimani kuomba na baadhi yao. Wale waliobaki
haohao WAKASHINDWA KUMTOA PEPO. Sababu kuu ni kuwa ndani yao kwa wakati huo
HAKUKUWA NA NGUVU inayozidi uwezo wa ile Mizizi ya pepo la kifafa kufanya
litoke. Na tunaona Yesu anawaambia NAMNA HII/STAILI HII/ NGUVU HII( ndani ya
pepo) haiwezekani kutoka isipokuwa kwa KUFUNGA NA KUSALI.
Hapo anataka
awaeleweshe kuwa sababu si kuwa yeye ni MWANA WA MUNGU ndiyo maana kaweza kutoa
pepo la hasha, Wala si suala la kiwango chao cha imani na ndiyo maana akasema
mbona hata mngekuwa na IMANI kama SIZE
ya punje ya HARADALI mngeweza Kuuambia mlima huu ng’oka hapa uende baharini nao
ungetii. Mathayo 17;20b-21.Lakini anawaambia kilichomsaidia ni kwa sababu
AMEFUNGA NA KUOMBA(AKAPATA NGUVU) ndiyo maana kaweza kumtoa Pepo la kifafa.
Kuna mahali pengine
anawaambia kuwa, mwanzo nilipowatuma, niliwaambia msibebe mkoba wala kanzu wala
panga, LAKINI SASA HIVI mwenye kanzu mbili amgawie mwenzake hali kadhalika
mwenye panga pia. ( Hapo alikuwa anazungumzia kwa namna ya ROHONI kuwa
wajipange kimaombi kwa sababu mbele yao kuna upinzani mkubwa kuliko nguvu
walizoenda nazo kwenye huduma iliyopita. NDIYO MAANA anasisitiza wakeshe pamoja
naye. Na hata yeye akiwa anaomba tunaambiwa malaika akaja akamtia NGUVU. LUKA
22;35 – 46.
MITHALI 24;10, “
UKIZIMIA siku ya taabu, NGUVU zako ni chache”.
Pia katika ZABURI 105;4, “anasema Mtakeni BWANA na NGUVU
ZAKE, utafuteni uso wake siku zote.”
Ukitumia MUDA MWINGI
kukaa na Mungu na kutaka NGUVU ZAKE itakusaidia sana kukufanya kutumia muda
mchache kutoa pepo, kuponya wagonjwa, kufufua wafu, kumiliki na kutiisha n.k
Ukikaa kwenye maombi
kwa dakika tano,kumi utakesha na pepo kwa masaa matatu ,kumi hadi siku kadhaa
na sauti kukukauka. Bali ukikaa muda mwingi na Yesu na kutaka NGUVU ZAKE,
utatumia SEKUNDE CHACHE kutatua tatizo lililopo katika ulimwengu wa roho na wa
mwili na pia kuamrisha kila kilicho kinyume chako.
YAFANYE MAOMBI KAMA NI
SEHEMU YAKO YA RATIBA NA MAISHA YA KILA SIKU NA SIYO KUFANYA KUWA NI TUKIO
MAALUMU. MUNGU ANATAMANI MARA NYINGI KUZUNGUMZA NA SISI, ANAHITAJI FURSA YETU
KUPITIA MAOMBI NA ANATAMANI AENDELEE KUTAWALA NCHI NA KILA KILICHOMO KUPITIA
WEWE.
OMBA MUNGU AKUPE NGUVU
NA KIU YA MAOMBI , UWEZE KUMILIKI NA KUTIISHA.
UHUSIANO
ULIOPO KATI YA MADHABAHU NA UHALALI WA
KUMILIKI NA KUTIISHA ARDHI / NCHI ULIYOPO
Madhabahu ni mahali
ambapo sadaka ya kuteketezwa (DHABIHU) inatolewa. Pia ni mahali mahususi pa
Mungu kusemezana na Mwanadamu na kuhojiana na vile vile ni mahali panapo pokea
muachilio wa Baraka za Mbinguni ( kutoka kwa Mungu) kumfikilia Yule ambaye anahusika
au kuihudumia hiyo madhabahu.
Mahali popote ambapo
kunafanyika ibada kuna madhabahu,, maana yake, kanisani, nyumbani, ardhini,
makaburini, ndani ya mwanadamu, maporini, kwenye mawe na kadhalika. Madhabahu
ni moyo wa hilo eneo hilo. Maana yake madhabahu
ya nchi ni moyo wa nchi. MOYO wa mwanadamu kwa mfano unafanya kazi ya kuachilia damu, chakula na
hewa kwenda sehemu nyingine zote za mwili. Pamoja na hilo hukusanya kila aina
za uchafu kutoka maeneo mbalimbali na kuupeleka unakohusika ili kutolewa nje ya
mwili. Moyo ni kiungo cha muhimu na ndiyo maana katika ulimwengu wa roho ni
bora mtu aweke jambo ulilo mfanyika kwenye akili yake kuliko aweke moyoni.
Mithali 4;23, “LINDA
sana MOYO wako kuliko yote uyalindayo, maana ndiko zitokako chemchemi za
uzima”.
Chemchemi za uzima
maana yake kila kinachohusu uzima ndani yako kinaachiliwa kutoka kwenye moyo na
kusambaa kuweka uzima maeneo yote yakuhusuyo.
Madhabahu ndiyo
yanayohusika kuachilia uzima fulani katika eneo ambalo yamewekwa. Madhabahu
inatoa kibali cha Ibada ya kimungu au ya kishetani kufanyika.
Tulikuwa
kwenye kanisa moja na marafiki zangu wa kiroho, Mungu akanisemesha juu ya
madhabahu ya kanisa lile na jinsi ambavyo shetani amebadilisha na kuruhusu
Ibada za kishetani, kafara za watoto wachanga, na kadhalika kufanyika. Tulikuwa
na maombi juu ya kukomboa nyakati za vijana zilizotekwa.
Na
katika kanisa hilo wazee tu ndo walikuwa washiriki wa Ibada mbalimbali hususani
fellowship n.k. tukaingia kuomba toba juu ya ile madhabahu na kuvunja kila
pando la adui na kufuta uhalali wa shetani na mawakala wake kutumia. Baada ya
hapo kukafuatiwa na Semina. Yaani ilifikia mahali wazee Fulani wakaanza
kulalamika na kusema hawa vijana wanataka kupindua kanisa.Yesu alitenda, mpaka
sasa vijana ndo wengi kwenye ibada za pale na baadhi ya wazee hatuwaoni tena.
Hususani ambao shetani aliwaweka makuhani kwenye madhabahu ile.
Madhabahu inafanya kazi
ya kuachilia vitu vya mungu wake kwa watu na pia inakusanya malemeo ya hao watu
na kutumia mifumo Fulani kutupa nje. Kuna vitu ambavyo Mungu akiachilia ni
lazima vipitie pekee katika Madhabahu ili vikufikie la sivyo, vinakwama. Kama
ilivyo kwenye moyo.
Katika Mwanzo 12;1 – 9,
anafafanua uhalali wa kumiliki kwa uwepo wa madhabahu
Tunasoma, “ BWANA
akamwambia Abramu, TOKA WEWE KATIKA NCHI
YAKO, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonesha nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza
jina lako, nawe uwe Baraka……………………................BWANA akamtokea Abramu,
akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko AKAMJENGEA MADHABAHU BWANA
aliyemtokea. Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; alikuwa
na Betheli upande wa Magharibi, na Ai upande wa mashariki, AKAMJENGEA BWANA
MADHABAHU huko ,akaliitia jina la BWANA.
Ukisoma sura ya 12 na
ya 13 katika kitabu hiki cha Mwanzo utaona kila mahali Mungu anapomkabidhi
Abramu kumiliki, Abramu anajenga madhabahu. Hii ni kwa sababu anajua fika
kwamba madhabahu ndiyo ambayo inampa uhalali way eye kumiliki mahali hapo
haijalishi kuna wageni wa aina gani na wenyeji mahali hapo.
MADHABAHU INAPEWA UHAI KWA SADAKA
YA KUTEKETEZWA ( DHABIHU) bila hivyo
madhabahu inabaki ni jengo tu. WARUMI 12;1
1WAFALME 18;21 – 46
hapa tunamuona Eliya akiwa na manabii wa mungu baali na tunaona anatafuta
kibali cha kujenga madhabahu kiaina. Lengo la Eliya ukisoma vema utaona sio
kushindanisha miungu na Mungu ila ilikuwa ni kutafuta mlango wa kupata kibali
cha kujenga madhabahu ya Mungu aliye hai, na ndiyo maana unakuta anaweka mawe
12 ili kuunganisha makabila yote kumi na mbili ya Isrraeli kwa madhabahu ile.
Na ili kuifanya madhabahu kuwa hai Eliya anaomba kuandaliwa ng’ombe kama
dhabihu ili aiteketeze kw moto juu ya madhabahu. Na baada ya shughuli zote
unakuta baada ya hapo anamwambia Mfalme Ahabu kuwa INUKA ULE UNYWE, MAANA KUNA
SAUTI YA MVUA TELE. Kumbuka ni mvua ambayo Eliya nabii aliizuia kwa Neno la
BWANA isinyeshe kwa zaidi ya miaka
mitatu. Sasa, ili mvua ile inyeshe tena juu ya nchi yao lazima iwepo madhabahu
ya kimungu kuruhusu mvua hiyo kunyesha. Kwa tafsiri nyingine Eliya anatafuta
uhalali wa kumiliki ile ardhi /nchi kupitia ile madhabahu atakayo ijenga ili
kuwepo na muachilio wa Baraka ya mvua tena juu ya ardhi hiyo.
KUMBUKA nilikuambia
kuwa; Madhabahu ndiyo inatoa uhalali wa umiliki wa ardhi, na ardhi ikimilikiwa
na adui inasababisha TOTAL DISCONNECTION( MTENGANIKO) kati ya ardhi hiyo na
Mungu, na kunapotokea hivyo anga la hiyo ardhi linakuwa linamilikiwa na MKUU WA
ANGA(PEPO). Na kazi yake kuu ni KUZUIA
kila kinachoachiliwa kama Baraka au majibu ya maombi ya watakatifu Mbinguni na
pia kutoa kibali cha ufalme wa giza kufanya kazi juu ya ardhi na watu na kila
kitu juu ya ardhi hiyo iwe ni wachawi, ibada za kipepo, baa, miungu, kafara,
vikao vya kipepo n.k. Shetani anapata kibali/ uhalali wa kuachilia magonjwa,
vifungo, roho za umasikini, ukichaa, kuvuruga ndoa za watu, kuteswa na
majinamizi usiku, roho za ajali, vifo vya ghafla,utoaji mimba, kafara, kufelisha
masomo n.k. DANIELI 10;3,13
Hapa huyu malaika
anasema , ……. “ tazama huyo mikaeli ,mmoja wa hao wakuu wa Mbele, akaja
kunisaidia; NAMI NIKAMWACHA HUKO PAMOJA NA WAFALME WA UAJEMI”.
Maana yake bado vita
inaendelea nah ii ni kwa sababu hawa wafalme au wakuu wa anga la uajemi bado
wanadai uhalali wao juu ya ile ardhi kwa maana hakuna madhabahu danieli
ameijenga kwa sadaka mahali pale. Ingawa
Katika SURA YA TISA YA KITABU CHA DANIELI tunaona Danieli akiomba toba juu ya
ardhi na watu wa Israeli na mlima mtakatifu wa MUNGU yaani madhabahu,, maana
yake anaondoa madhabahu na mapando juu ya ardhi yao ya kipepo lakini hatuoni
mahali akitoa Sadaka ya kuteketezwa juu ya madhabahu ya Bwana ili kuachilia
UHALALI wa umiliki wa ardhi ile juu yao.
Shetani akijenga madhabahu
katika eneo la shule haijalishi walimu wanafundishaje na wanafunzi wanajituma
vipi, roho ya kufeli itawasumbua sana wanafunzi HATA WALIOOKOKA ( WATEULE).
Madhabahu ya shetani ikikalia nchi haijalishi uongozi ni mchapa kazi vipi au
mfumo wa kiutawala ukoje. Lazima hata hivyo ataachilia vitu vya kwake. Kiongozi
awe mzuri kiasi gani hawezi kuzuia ajali kutokea, hawezi zuia vifo mbalimbali
kutokea, hawezi kuzuia majanga na balaa katika nchi, hawezi zuia uchumi
usishuke. Ni madhabahu peke yake juu ya nchi ndiyo inayo achilia au kuzuia
mabaya kutegemeana na aina ya mungu wa madhabahu hiyo.
Ndiyo maana neno
linasema kama MISINGI IKIHARIBIKA( MF. MADHABAHU YA MUNGU ) mwenye haki
atafanya nini???. Zaburi 11;3.
Tutaomba wee kwaajili
ya familia, mashule na vyuo, nchi, makazi, ajira, ndoa, biashara n.k lakini
tusipojua msingi wa kimadhabahu katika maeneo hayo ulivyo na kujenga madhabahu
ya kimungu, tutakuwa tunajilisha upepo.
Kumbuka; unapobomoa,
kuharibu na kuangamiza jua pia kuna kujenga na kupanda. Usiishie tu kuvunja na
kuharibu madhabahu za giza(shetani) bali pia kumbuka zaidi KUJENGA NA KUPANDA
madhabahu ya Kimungu katika jina la Yesu. Yeremia 1;10.
2 nyakati 1;6 – 7, “…
Suleimani akaipandia huko madhabahu ya shaba mbele za BWANA , iliyokuwako
hemani pa kukutania, akatoa sadaka elfu za kuteketezwa ( DHABIHU) juu yake.
Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani, akamwambia, OMBA UTAKALO NIKUPE”.
Hapa tunaona kilichompa
uhalali na kibali Sulemani cha kuambiwa kuomba analotaka (LOLOTE) ni madhabahu
iliyotiwa uhai kwa sadaka aliyotoa na ndipo akapata muachilio wa aina zote za
Baraka atakazo zitaka. Mara ngapi Mungu anasema na wewe omba utakalo nami
nitakupa???. Kuna mambo mengine hayaendi bila yaw ewe kuihudumia madhabahu.
Tukisisitiza utoaji kanisani au katika huduma unahisi kuwa hawa watumishi siyo
bure, wanataka walee pesa zetu ama vitu vyetu, bila kujua kuwa unafuta uhalali
wa Mungu kukumilikisha ardhi yako kupiitia madhabahu. YAANI NIKWAMBIE
ukiihudumia vema madhabahu (KWA SADAKA YA KUTEKETEZWA INCLUDING MWILI WAKO [
WARUMI 12;1]) unafanya Mungu akose namna atalazimika tu kukwambia sema lolote(
Mali, utajiri, mume/mke, watoto, kazi, cheo, ufaulu, uponyaji, kufunguliwa,
n.k) name nikupe. NA HAKIKA YAKE ATAKUPA. Maana huo ndiyo mfumo aliouweka wa
muachilia wa chochote kwako mwanadamu
Lakini kumbuka pia
PASIPO IMANI haiwezekani kumpendeza Mungu, Maana kila amwendeaye Mungu LAZIMA
(SIYO HIARI) aamini kwamba yeye yupo na kwamba HUWAPA THAWABU wale wamtafutao.
WAEBRANIA 11;6.
Usitoe mchango wa
jengo, toa sadaka ya jengo, Usitoe Mchango wa Maendeleo ya Dayosisi toa Sadaka
ya maendeleo ya dayosisi, UNANIPATA SAWASAWA????
Makanisa mengi
yanatumia neno mchango kwenye sadaka mbalimbali ndiyo maana watu hulalamika
kuwa duh leo siendi kanisani michango imezidi. Lakini ungekuwa unatoa kama
Sadaka usingekuwa unalalamika maana unajua mpokeaji ni Mungu na lazima
atafungulia madhabahu kuachilia chochote utakachoomba. KWA MAANA HAZINA yako
ilipo, ndipo utakapokuwako na moyo wako (MADHABAHU). Mathayo 6;21.
Hili
somo linamhusu sana mtu aliyeokoka, KAMA haujaokoka na unatamani ujiunge katika
familia ya Mungu ili upewe uhalali wa
KUTAWALA NA KUMILIKI NCHI kwa njia ya Maombi fuatisha sala hii kwa IMANI.
Tafuta MAHALI PA
UTULIVU na Sema sala hii pamoja nami kwa Roho na kweli kutoka ndani ya moyo
wako;
“Bwana
Yesu, ninakushukuru kwa Rehema na fadhili zako nyingi ulizozionesha pale
ulipojitoa na kufa msalabani kwa ajili yangu mimi mwenye dhambi.Ninakuja kwako,
ninaomba unisamehe dhambi zangu zote na unipokee, futa jina langu katika kitabu
cha mauti, na uliandike kwenye kitabu cha uzima; unipe uwezo wa kufanyika
mtoto wako tangu sasa. Ninajiachilia
kwako, uwe BWANA na mwokozi wa maisha yangu; unitawale katika mwili, nafsi na
roho yangu, nikatembee katika mapenzi yako siku zote za maisha yangu.Asante kwa
kuwa tangu sasa nimeokoka na kuwa kiumbe kipya. Ya kale yote yamepita na
tazama,yamekuwa MAPYA, katika jina lenye NGUVU na MAMLAKA, jina la YESU
ninaomba na kuamini kuwa nimepokea sasa.AMEN!!!
Baada ya kusema sala
hii amini kuwa upo ndani ya Yesu naye yuko ndani yako. Endelea kuishi katika
misingi ya utakatifu katika kujifunza Neno lake na maombi huku ukiufurahia UZURI wa Yesu usiochakaa ndani ya
wokovu huu aliokupa.
KISHA FANYA MAOMBI KWA
MWONGOZO HUU;-
1.
INGIA KATIKA MAOMBI JUU YA ENEO ULILOPO
NA WATU WA ENEO,,
2.
TUBU KWA AJILI YAO NA KWA AJILI YA ENEO
AMBALO UMEWEKWA AU UPO IKIWA NI PAMOJA NA UZINZI, RUSHWA, UCHAWI NA USHIRIKINA,
UMWAGAJI DAMU ISIYO NA HATIA, UZURUMAJI N.K,,
3.
HARIBU KILA MIFUMO YA KIUTAWALA AMBAYO
SHETANI ANAIWEKA KATIKA ARDHI HYO IKIWEMO WACHAWI,WAGANGA, MAPEPO, MAJINI,
MIZIMU N.K
4.
RUHUSU MUUNGANIKO (RE-CONNECTION) KATI
YA MBINGU (NA KILA KINACHOACHILIWA) NA ARDHI ULIYOPO
5.
KATAA KILA HALI ISIYOKUWA YA UFALME WA
MUNGU MAHALI ULIPO KAMA VILE MAGONJWA, VIFO, KUIBIWA, MAJANGA, UMASKINI,
KUTESWA NA MAPEPO/ KUFUNGWA, KUTOKUZAA, KUTOKUOLEWA/ KUOA, KUTOPATA KAZI,
KUTOFANIKIWA, ARDHI KUZAA MIIBA NA MICHONGOMA N.K
6.
TUMIA DAMU YA YESU NDIYO INAYOKUPA
UHALALI WA KUMILIKI KIFALME KATIKA ULIMWENGU WA ROHO MAHALI ULIPO..
WARUMI 8; 31, “ Basi
tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo UPANDE WETU ,ni nani aliye JUU YETU?”
MWISHO!!!!
KWA HUDUMA, MAOMBI NA
USHAURI ;
www.urejesho.
Blogspot.com
Email; nicksonkp@gmail.com
Simu no; 0757 35 05 27
au 0717 23 64 90
HUDUMA YA MAOMBI YA
UREJESHO
Comments
Post a Comment