KAZI YA DAMU YA YESU ILIYO ACHILIWA MWILINI MWAKE.



1.KUFANYA AGANO JIPYA KATI YA MWANADAMU NA MUNGU.

**Agano jipya ni Imara zaidi lihusulo WOKOVU kwa NEEMA kwa njia ya IMANI
**Limefanyika kwa damu ya Yesu inenayo MEMA kuliko damu nyingine Zote.
-inanena:-UPONYAJI,UZIMA,WOKOVU,MAFANIKIO nk.
**Imetolewa na Yesu mwenyewe kama KUHANI MKUU.Ebr 4:14-16.

2.DAMU KUTOKA KICHWANI MWAKE

a).Damu iliyotoka kama jasho. Luka 22:44

>>LENGO:-
....Kufuta laana ya KULA KWA JASHO.Mwa 3:19,hagai 1:6-7.
*kutumia nguvu sana kunafanya jasho kitoke.MEANS: MTATUMIA NGUVU NYINGI BILA MAFANIKIO MAANA HAMNA MAARIFA.
-ndiyo maana wakristo wengi wanaishi kwa madeni HAWANA MAVUNO jambo ambalo siyo mpango wa Mungu kabisa.KUMBUKA: IPO TOFAUTI KATI YA MKOPO NA DENI!

*Kwanini damu kama jasho imwagike kichwani???
-(KUTENGENEZA KWA UPYA MFUMO WA AKILI<ubongo> ili mwanadamu aweze kufikiri kwa undani kuliko kufanya mambo mengi yasiyo hata na mafanikio

b).Damu kutoka kichwani mwake kwa TAJI YA MIIBA.Math 27:29.

>>LENGO:-
**Kufuta laana juu ya ardhi.Mwa 3:17-18
-Ukiona shamba lako halitoi mazao inavyostahili ACHILIA DAMU YA YESU.
KUMBUKA: chochote ambacho kuna kitu kinapandwa juu yake ili kutoa zao fulani/kitu kipya TUNAKIITA SHAMBA
MFANO:
¤TUMBO LA MWANAMKE-usitafute mwanamke mwingine uzae nae eti mke wako hazai ACHILIA DAMU YA YESU KWENYE HIYO MICHONGOMA
¤MIFUGO
¤SADAKA YAKO
¤BIASHARA n.k.

3. DAMU YA YESU KUTOKA UBAVUNI MWAKE.Yohana 19:34,37
(UBAVU KWA TAFSIRI NYINGINE KIBIBLIA NI MWANAMKE).

>>LENGO:-

a). Uponyaji wa FAMILIA kupitia MWANAMKE

**KUMBUKA:Mungu alipitisha mwanawe kwenye tumbo la mwanamke ili kuponya udhaifu wa mwanamke

**FAHAMU HILI PIA:UASI ulipitia kwa mwanamke ambaye ni UBAVU, hivyo damu inapoachiliwa ubavuni ni kumtoa yeye na uzao wake katika laana na udhaifu wa dhambi.

SIKILIZA: Huo mpango wa haki sawa wakati mwingine unatafsiriwa kinyume na Mungu kabisa

NENO LINASEMA;
1.MWANAMKE atamtii MUME WAKE
2. MWANAMUME atampenda MKE WAKE.Kolosai 3:18.

b).Uponyaji wa KANISA
**KANISA ni limefananishwa na bibi harusi(mwanamke) na Yesu akiwa Bwana harusi.LUKA 12:35-36
>>MILANGO YA KUZIMU HAITALISHINDA KANISA.
**Hatujatambua nguvu iliyopo ndani ya DAMU YA YESU ndiyo maana MAAJENTI WA SHETANI,WACHAWI NA NGUVU ZA KUZIMU vikitutisha,tunatishika.TUFUNGUKE SASA KANISA LA TANZANIA NA ULIMWENGU NA TUACHILIE DAMU YA YESU.HAKIKA IBILISI NA MAWAKALA WAKE WATATIMUKA!OOH HALELUYA!!!

4.DAMU MWILINI KWA KUPIGWA NA MIJEREDI.Isaya 53:4-5

>>LENGO:-

**Kuachilia uponyaji katika maeneo yote.
K.M:-
1).UPONYAJI WA DHAMBI(MOYO).Yere 17:9-10.

2).UPONYAJI WA MAGONJWA(sehemu zote za mwili).

3).UPONYAJI WA BIASHARA, UCHUMI, ELIMU, AFYA, MALI, HUDUMA NDANI YA KANISA N.K.

POKEA MAOMBI HAYA SASA: "Baba katika jina la Yesu, ninakuja mbele zako kama kuhani ninaachilia DAMU YA YESU juu ya msomaji wangu, Ikamtakase na kuondoa dhambi na laana juu yake, familia, kazi, ardhi na chochote alicho nacho.NINAACHILIA DAMU YA YESU KUMLINDA NA KUMPONYA NA MABAYA YOTE.NINAACHILIA DAMU YA YESU KUMPA AMANI NA FURAHA KWENYE MAISHA YAKE YOTE KATIKA JINA LA YESU" Sema AAMEEN....!!!

Na:mwl.N.Kipangula-HUDUMA YA MAOMBI YA UREJESHO.
Email: kipangulanickson@yahoo.com
Phone: 0757350527

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KURUHUSU UTUKUFU (GLORY) WA BWANA KUFANYA JAMBO KATIKA MAISHA YAKO