NAMNA
YA
KULILINDA KUSUDI LA MUNGU
YAJUE MAMBO YATAKAYO KUSAIDIA KUISHI
KWA FAIDA DUNIANI ILI KUJIWEKEA HAZINA NA MAHALI MBINGUNI
NA; MWL. NICKSON KIPANGULA
YALIYOMO
1.
Shukrani………………………………………………………………………………….3
2.
Maana
Na Umuhimu Wa Kulilinda Kusudi ………………………………..4
3.
Kubadilishwa
Kwa Kusudi Toka Ulimwengu Wa Roho(Sirini) Mpaka Ulimwengu Wa
Mwili……………………………………………………………......................11 - 13
4.
Umuhimu
Wa Kuomba Kwa Mzigo ( Maombi Mazito) Yanayokufanya Ulilinde Kusudi Na Kutembea
Ndani Yake……………………………13 - 14
5.
Wafahamu
Watu Na Kabila Za Watu Wanaotolewa Punde Unapokuwa Wa Thamani(Kusudi
Linatembea/Linaishi) Machoni Pa Mungu………………………………………………………………………………………15
6.
Nguvu
Ifanyayo Kusudi La Mungu Kudhihirika (Kuwa Halisi)………………………………………………………………………………16
- 17
7.
Mambo
Yatakayo Kusaidia Kulilinda Kusudi La Mungu..18 - 19
8.
Mwisho…………………………………………………………………………20
SHUKRANI
Shukrani
zimwendee Mungu aliye hai anipaye pumzi ya uhai na bubujiko la kimaandiko kwa
ajili ya uponyaji wa watu wake. Nasikia
raha, kukutumikia ee Baba katika Kristo Yesu!!
Aidha
shukrani ziwaendee wote wanaobeba mzigo kuomba juu ya watumishi waliobeba
kusudi la Mungu kuendelea kusambaza habari njema ya Ufalme wa Mungu, Kazi yenu
si bure katika Bwana. Mtalipwa kwa wakati.
“Ujumbe huu ukufanye ubadilishe fikra,
ufahamu na roho yako kumwelekea Mungu katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti,
AMEN!!! KARIBU!!!!!!!!!!!”
KUSUDI (purpose)
– kitu kilichokufanya uwepo ulipo au kuja kuwepo utakapokuwa.
Hakuna kitu kilichopo mahali bila kusudi na hakuna kitu
kilichoumbwa pasipo kusudi na pia hata wewe usingekuwepo ulipo bila kusudi. Upo
Tanzania,au kwenye mkoa ulipo kwa sababu lipo kusudi Fulani ambalo linatakiwa
kutimia tu wewe unapokuwepo pale na bila wewe ni ngumu likatimia.
Lipo jambo ambalo ni maalumu (so specific) linalokufanya
uwepo mahali ulipo. Hakuna mwanadamu aliyeachiliwa azaliwe bila kuwepo na
kusudi la kuwepo kwake duniani la sivyo, asingezaliwa.
Vipo vitu vingi sana ambavyo wewe unataka uvifanye kwenye
maisha yako, pia vipo vitu vingi sana ambavyo Mungu anataka wewe uvifanye
kwenye maisha yako, vilevile vipo vitu vingi sana ambavyo shetani anataka wewe
uvifanye kwenye maisha yako. Kamwe huwezi kuvifanya vyote. Unafanyaje kujua ni
kitu kipi ambacho Mungu anakutaka ukifanye kwenye maisha yako? Au ilimradi kipo
kwenye ufahamu wako basi unafanya!!!
Unapotambua wewe ni nani sasa na baadaye na ni kwa kusudi
lipi upo utakuwa makini (SERIOUS) – UKIUKOMBOA WAKATI. Maana bidii ya ndani
itajengeka na kukufanya uanze kuyaandaa mazingira ya kulitimiza hilo kusudi.
Hautakaa kupoteza muda kwa mambo ambayo hayahusiani na kusudi ulilopewa
kulitimiza duniani. Watu wengi utasikia anasema ngoja niende kwa rafiki yangu
nikapoteze MUDA, haujalijua kusudi wewe!!!
Waefeso 5:10,15-17 biblia inasema, “…mkihakiki ni nini impendezayo Bwana……………….Basi angalieni sana jinsi
mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
MKIUKOMBOA WAKATI kwa maana zamani hizi ni za UOVU. Kwa sababu hiyo msiwe
wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana”.
Tutafakari kidogo hapa;-
1. Mkihakiki ni nini impendezayo Bwana-
hapa anataka tuone kuwa siyo kila kitu utatakiwa kukifanya hata kama una uwezo
wa kukifanya na hata kama siyo dhambi kukifanya. KUHAKIKI maana yake ni kujipa
uhakika Fulani juu ya jambo Fulani lililoko mbele yako kwa lugha nyingine ni
kuamini. Na kuamini kunatokana na Neno la Mungu na pia ukumbuke kuwa Neno la
Mungu ndiyo mapenzi ya Mungu. Hii ina maana ya kuwa kitu chochote unachotaka
ukifanye ni lazima ukipitishe kwenye Neno la Mungu ili kupata uhakika kama ni
mapenzi ya Mungu kukifanya au la.
2. MKIUKOMBOA WAKATI kwa maana zamani
hizi ni za UOVU- Fahamu kuwa huwezi ukakomboa kitu kama hakijatekwa. Hii
inamaanisha kuwa kuna kitu ambacho kimeuteka WAKATI ndio maana wakati unahitaji
kukombolewa. Kitu hicho ni UOVU. Unapofanya uovu maana yake unapoteza wakati
aliokupa Mungu wa kutimiza kusudi alilokupa.Mfano upo kwa rafiki yako
mnamsengenya mtu wakati Mungu alikutaka muda huo uwe mahali Fulani unamshuhudia
mtu Fulani Neno la Mungu,au upo na mtu kufanya uzinzi na kumbe wakati huo
ulipangwa na Mungu uwe mahali Fulani unamuombea mgonjwa Fulani kumnusuru na
roho ya mauti inayotaka kummeza ambapo inawezekana wewe ndiye mtu PEKEE wa
kumwombea asife. Kumbuka kila sekunde imehesabiwa kwa wewe kufanya jambo Fulani
na usipojua kuwa kwa wakati Fulani ulitakiwa kufanya jambo Fulani maana yake
utafanya jambo lisilo kwa ule wakati. YOUR
TIME IS SO FIXED kiasi kwamba hakuna dakika za majeruhi kama kwenye mpira
wa miguu. La sivyo, Mungu aamue mwenyewe kukuongezea muda kwa rehema kama
ilivyokuwa kwa mfalme Hezekia (Isaya
38:1 – 6).
Anamwambia Tengeneza mambo ya nyumba yako MAANA
utakufa wala hutapona na hajasema usipotengeneza utakufa. Hii ina maana ya kwamba
kutengeneza au kutotengeneza mambo ya nyumba yake hakuathiri kufa kwake ila
awaache wakiwa na mwelekeo, maana yake kama ni mirathi,wosia n.k ndio wakati wa
kutoa maana punde baada ya huo ugonjwa kinafuata kifo. Na unakuta baada ya
kuomba anaambiwa nitaziongeza siku zako kiasi cha miaka kumi na mitano maana
yake zilikuwa zimeisha. Hii ni kwa watu wachache sana yaweza kutokea.
Kwa mfano;-
Ukijua kuwa baadaye utakuwa mhubiri wa
kimataifa;
1. Maombi yako mara nyingi yatakuwa kwa
kiwango cha kimataifa.maana yake utakuwa unatazama maombi yako kwa kiwango cha
kimataifa.
2. Utakuwa unafanya bidii ya kujua lugha
mbalimbali za mataifa mbalimbali.
3. Utakuwa unafanya mazoezi ya kuhubiri
hata ukiwa peke yako au ukiwa na marafiki utakuwa unatamani uwe unawahubiria tu
bila kuongea mambo mengine.
Hebu tusome hapa; Marko 11:12-14,20, “Hata asubuhi yake walipotoka Bethania aliona
njaa. Akaona kwa mbali mtini wenye majani,akaenda ili labda aone kitu juu yake;
na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa tini. Akajibu
akauambia, tangu leo mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake
wakasikia………………….Na asubuhi walipokuwa wakipita, waliuona ule mti umenyauka
toka shinani”.
Sasa hapa tulia kidogo nichimbe;
Anaposema aliona njaa maana yake alihitaji chakula. Na kufuatana
na Injili ya Yohana 4:30 – 38, chakula kinachoshibisha njaa ya Yesu ni kuona
mapenzi ya Mungu yanatendeka na kazi(kusudi) aliyotumwa na baba yake inatimia.
Sasa twende pamoja; Anapouangalia mtini anauona umechanua majani (
unachangamka, unasifu na kuabudu, unatoa
sadaka, unafanya maombi hata kufunga,unanena kwa lugha, una imani ya kuhamisha
milima n.k) kwa hiyo anatarajia apate kitu kwake, na kumbuka hajasema apate
tunda amesema kitu. Kuna aina ya KITU ambacho Yesu anatafuta kwa ule mtini
ambacho kinatakiwa kuwepo kwa ule wakati/msimu. Anapousogelea anasema hakuona
kitu ila majani. Na nataka uelewe kuwa lile neno “MAANA SI WAKATI WA TINI”
Limetamkwa na ule mtini na hii ni katika kujitetea kwa Yesu. Maana tunaambiwa
Yesu AKAJIBU akauambia………. Asingeweza kujibu kama hajaulizwa swali nao. Na hii
inaonesha haya yalikuwa ni mabishano katika ulimwengu wa roho kati ya ule mti
na Yesu. Na inaonesha baada ya ule mtini kuulizwa kuwa mbona umepata neema ya
kumwagiliwa maji na kutiwa mbolea hata umekuwa na majani umechanua lakini
hutaki kuzaa matunda ninayotaka? Na huo mti ukaongeza swali kwa Yesu kuwa,
mbona huu sio wakati wetu akina tini kuzaa matunda? Ndio maana tunaambiwa Yesu
akajibu akauambia mtini tangu leo mtu asile matunda kwako. Walipopita asubuhi
inayofuata wakakuta umenyauka toka shinani.
Sikiliza, Mungu anapokufanikisha anakupa, kazi, pesa, mke,
watoto, nyumba, gari, imani, upako n.k nia yake ni kuona unafanikisha kusudi
Fulani ambalo ameliweka ndani yako. Inawezekana hata wewe mpendwa unasema huu sio
wakati wangu wa kutumika labda mpaka nimalize shule au nikioa/kuolewa au
nikishapata watoto, au nikipata kazi Fulani. Mwingine unasema nitaokoka kwenye
mkutano mwingine wa injili kama huu ukija mwakani.
Unapolikubali kusudi la Mungu na kulilinda Mungu
anakuheshimu kwa kiwango cha juu sana na kukuona wa thamani. Punda na
mwanapunda ambao walitumika na Yesu katika kusudi la kumfikisha Yesu Yerusalemu
wasingefunguliwa na wangebaki wamefungwa na pia wasingelitembea juu ya zile
nguo watu walizotandika kama wasingelikubali kutumikia lile kusudi. Luka 19:29 – 36. Wapo watu waliuliza
mbona mnamfungua mwanapunda? Wakasema, Bwana anamhitaji. Inawezekana ni ndugu
zako ndio vizuizi vya wewe kutembea kwenye kusudi la Mungu ama ni wazazi,
wanakuzuia kutumika kwa Bwana. Semezana nao katika namna ya maombi waambie
Bwana ana haja na mimi niachieni nimtumikie katika jina la Yesu. Lazima tu
watakuachilia.
Luka 2:40, “Yule mtoto (YESU) akakua, akaongezeka NGUVU,
amejaa HEKIMA, na NEEMA YA MUNGU ilikuwa juu yake”.Hakuna jambo lisilo
na mwanzo lazima kuwe na UKUAJI(GROWTH) na KUONGEZEKA(DEVELOPMENT). Huwezi
ukaanza tu kufanya semina za kufunga MAHEMA au huduma za nchi za nje wakati
kuweza kuhubiria hata watu kumi huwezi bado. Au unategemea uwe daktari bingwa
wa upasuaji wakati hata kupasua vyura au mende inakushinda. Au eti uwe waziri
wakati hata uenyekiti wa kijiji watu wanakukataa. Lazima ufahamu namna ya
kujipanga mwanzo wake. Lazima ukue kimawazo,kifikra na kimtazamo juu ya kusudi
ulilopewa ndipo Mungu akupe NGUVU akujaze HEKIMA yake na NEEMA yake ikae juu
yako. HEKIMA ni ya msingi kumbuka mwanzo tumesema ili utimize kusudi la Mungu
lazima uweze kuukomboa wakati na hauwezi kuukomboa wakati kama haujaenenda kama
mtu mwenye HEKIMA.Haleluya!!!!!!!!!!!!!
Yesu katika hali ya kawaida alizaliwa kama mimi na wewe
tulivyozaliwa. Ingawa alikuwa Mungu lakini tangu anazaliwa anajua kusudi la
Mungu ni nini, kwa hiyo hakuishi kizembe kizembe. Kukua hata kama hupendi
utakua tu. Tunaambiwa Yesu akaongezeka NGUVU, HEKIMA na NEEMA YA MUNGU. Vitu
hivi haviji tu lazima kuna bidii inayohitajika ndani yako ambayo inakufanya
upate hiyo HEKIMA. HEKIMA ni kuwa na uwezo wa kupambanua mambo ili kujua lipi
ni sahihi na lipi siyo sahihi. Na Hekima ni juu ( BEYOND ) ya AKILI / UELEWA wa mwanadamu. Na ndiyo maana
mtu anaweza akawa na akili sana au amesoma sana lakini akakosa HEKIMA.
Kwani hujaona wewe, madaktari ambao wanajua kabisa kuwa
pombe na sigara vina madhara makubwa mno kwa afya ya binadamu, ikiwemo mapafu,
maini, figo, mishipa ya damu,kisukari, vidonda vya tumbo n.k lakini ni
watumiaji kupindukia??? HEKIMA iko wapi???? Wana akili lakini wamekosa hekima.
Kuna process (mchakato ) ambao Yesu alikuwa akifanya katika
ulimwengu wa roho kutafuta HEKIMA ya Mungu. Hekima inatafutwa kwa bidii.
Mithali 8:12,17. Yesu alikuwa na
kuongezeka kwa sababu alikuwa anajua hapa lazima nifikie KIWANGO Fulani cha
HEKIMA, NGUVU na NEEMA YA MUNGU ili niweze kutimiza KUSUDI la Mungu
aliloniwekea duniani.
Yesu angekosa Hekima na Neema ya Mungu yamkini angeweza
kufanya akamatwe mapema hata kabla hajawaandaa watu kabla ya kufa kwake.
Angekosa NGUVU ya kiwango Fulani inawezekana angeshindwa kuyabeba MATESO ambayo
yalikuwa juu yake.
Elewa kitu hiki; ukiondoa Mungu, kila kitu kina mwanzo wake.
Watu husema , “Mbuyu nao ulianza kama mchicha”.
Hebu turejee kitabu cha Yohana 1;1-3 nayo inasema, “ Hapo
mwanzo kulikuwapo na NENO naye NENO alikuwapo kwa Mungu, naye NENO alikuwa ni
Mungu. Huyo(NENO) mwanzo alikuwa kwa Mungu, vyote vilifanyika kwa huyo(NENO)
wala pasipo yeye (NENO) hakukufanyika chochote kilichofanyika”.
Hapa napenda uelewe kitu hiki; anaposema hapo mwanzo ina
maanisha ni mwanzo wa kitu Fulani. Na anataka kutueleza kuwa kuna aliyekuwepo
kwenye huo mwanzo wa hicho kitu Fulani ili kufanya kitu Fulani kitokee na
pasipo yeye kisingewezekana kutokea. NENO ndiye aliyekuwepo kwenye hiyo mwanzo
na ndiye aliyefanya vitu vyote kufanyika kwa yeye ( vinavyoonekana na visivyoonekana). Kwa Mujibu wa Yohana
1;14,ambapo inasema, “Naye NENO
akafanyika mwili, akakaa kwetu, nasi tukauona utukufu wake. Utukufu kama wa
mwana wa pekee atokaye kwa baba, amejaa neema na kweli” ni dhahiri kuwa
anazungumza kwa habari za NENO kama YESU.
Labda tuangalie kidogo mfumo wa uumbaji ambao Mungu
alitumia kuumba vitu vyote kama unavyojionesha katika kitabu hiki cha Mwanzo 1;
1-3 ambapo inasema, “ Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi, nayo nchi ilikuwa ukiwa
tena utupu. Roho ya Mungu ikatulia kwenye vilindi vya uso wa maji. Mungu
akasema(NENO), na iwe nuru ikawa nuru.Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema. Ikawa
jioni ikawa asubuhi siku moja”.
Sasa hapa anaposema “……Roho ya Mungu ikatulia juu ya vilindi vya
uso wa maji…….” ana maana kuwa Roho anasubiri ushirika Fulani.
Na ndiyo maana tunaona Mungu Baba akimwachilia NENO(YESU) kumruhusu Roho
mtakatifu kuambatana naye ili kwenda kufanya Nuru iwepo.
Watu wengi huwa wakifikiri juu ya makusudi kwenye maisha
yao wanakata tamaa hususani wanapowazo namna wani wataweza kulifikia kusudi na
kutembea ndani yake. Lakini hapo tunaona wazi kuwa Roho mtakatifu hutulia
kilindini pa uso wa maji( mahali pa utulivu ) ili kusubiri kusikia sauti ya
Mungu( NENO ) ili atende kile NENO anasema ama kutoa mwongozo.
Ili Roho Mtakatifu ayatendee kazi maombi yako ni lazima
yaambatane na NENO na si kelele maana ana maana nzuri tu kukaa kwenye vilindi
vya uso wa maji anatafuta utulivu. KELELE tafsiri yake ni maombi ya mwenye
dhambi.
BIBLIA inasema, “Maombi ya mwenye dhambi ni kelele mbele za
Mungu..” Maana yake ni kwamba unapomuendea Mungu kwa lengo la kupeleka maombi
mbele zake sharti ujue Roho takatifu hatavumilia maombi yasiyoambatana na Toba
ikiwa mwombaji haujajitakasa.
Pia ufahamu kuwa Roho mtakatifu hatii maombi ilimradi
yameombwa na mtakatifu ila anatii tu maombi ambayo yamebebwa na NENO ndani
yake( Holy Spirit doesn’t respond to any prayers BUT he only respond to the
prayers contented with The WORD OF GOD). Ndiyo maana hata Yesu
anawaambia wanafunzi wake katika Yohana 6; 24, “……Hata sasa hamjaomba NENO lolote
kwa jina langu. Ombeni, nanyi mtapewa ili furaha yangu iwe timilifu”.
Utashangaa ni kwanini anawaambia hawajaomba wakati kila mara anapanda nao
mlimani kuomba?? Jibu ni hili, Yesu anawaambia hawajaomba NENO, inawezekana
wameomba maombi mengi sana lakini hayajabeba NENO ndani yake.
Haiyamkini, hata wewe umekuwa ukiomba sana mipango yako
maishani ipate kutimia na umekuwa ukimlilia Mungu muda mwingi lakini huoni
matokeo au udhihirisho wa maombi yako. Fahamu kuwa NENO LA MUNGU ndiyo MAPENZI
YA MUNGU na ndiyo MAKUSUDI YA MUNGU. Lazima maombi yako yajae kwenye mpango wa
Mungu, au makusudi ya Mungu la sivyo
utabaki kusema mbona Mungu unasema maandalio ya moyo ni ya mwanadamu??? Lakini
anasema bali jawabu la ulimi( NENO ) linatoka kwa Mungu. Jizoeze kupitisha
kwenye NENO la Mungu jambo lolote kabla hujaliomba. Na biblia inasema kila NENO
la Mungu limehakikishwa,yeye ni ngao yake amwaminiye.
Kumbuka; Sababu ya wanafunzi kutomwacha Yesu kabla
hawajajua kuwa ni Mungu ni kwa sababu ya NENO lake. Yohana 6;66-69, “…….Basi Yesu
akawaambia wale Tenashara, Je, na ninyi mwataka kuondoka? Basi Simoni Petro
akamjibu, Bwana! Twende kwa nani(mwingine)? Wewe unayo MANENO ya UZIMA WA
MILELE……”
KUBADILISHWA KWA KUSUDI TOKA ULIMWENGU WA ROHO(SIRINI)
MPAKA ULIMWENGU WA MWILI
Ili kulifahamu kusudi na kutembea ndani ya hilo kusudi
lazima uingie katika ulimwengu wa roho ili ufahamu ni nini ambacho kipo kwa
ajili yako au wewe upo kwa ajili ya nini katika ulimwengu wa dunia hii. La
sivyo unaweza ukaishi nje ya kusudi au ukafa kabla ya wakati wako kwa sababu
Mungu hawezi kukuvumilia wewe ambaye unaishi bila kuwa ndani ya kusudi. “Kila tawi ndani yangu lisilozaa (matunda)
huliondoa, na kila tawi lizaalo hulisafisha ili lizidi kuzaa”.Yohana 15;2
Wapo malaika ambao wanatembea na wewe siku zote ndio ambao
wana kutathmini( evaluate) mambo unayoyafanya kama yapo ndani ya kusudi au la.
Halafu wanapeleka ujumbe kwa Mungu kuwa huyu mtu ni kweli yupo duniani
anaishi,anakula, anafanya kazi n.k lakini hata sasa miaka 10,15,30 au zaidi
aliyo nayo bado yupo nje ya kusudi lako.
Fikiria, kama wewe unataka kujenga nyumba ya ghorofa mbili
kwa mwaka mmoja na umewatafuta mafundi ambao unajua watakujengea, na ukawapa
vifaa vyote vya ujenzi badala yake baada ya miezi nane unapokagua maendeleo ya
jingo ukakuta wamejenga kijumba chenye chumba kimoja au wameshikilia tu fedha
na vifaa vya ujenzi wala hawana habari, utawafanya nini?
Yeremia 1:11-12 inasema,
“ Tena neno la BWANA likanijia, kusema,
Yeremia, waona nini? Nikasema naona ufito wa mlozi. Ndipo BWANA akaniambia,
Umeona vema, kwa maana ninaliangalia neon langu, ili nilitimize”. Baada
ya Yeremia kuona ufito wa mlozi NDIPO Bwana anamwambia umeona VEMA, maana
ninaliangalia Neno langu ili nilitimize maana yake asingeona vema asingejua kama
Mungu analiangalia Neno lake( neno lililobebwa ndani ya tafsiri ya UFITO WA
MLOZI).
Ilimpasa Yeremia aingie katika ulimwengu wa KIMAONO ili
aweze;-
1. Kuona kile Mungu anamwonesha (UFITO WA
MLOZI)
2. Kujua tafsiri yake (HUO UFITO WA MLOZI UNAVYOMAANISHA)
KUMBUKA; Pasipo MAONO watu huacha kujizuia(wanaangamia)
Mithali 29;18-19.
When you live with VISION;-
You will not go ANYWHERE but you
will go to the SPECIFIC SOMEWHERE,
You will not live with ANYONE but
you will live with the SPECIFIC SOME ONE,
you will not do ANYTHING but you
will do the SPECIFIC SOMETHING,
because what you SEE is what you are
DOING..Haleluyaaaa…..!!!!!!!!!!
Isaya 45;3, “….nami nitakupa wewe hazina za gizani, na mali
zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA nikuitaye kwa
jina lako, naam, Mungu wa Israeli ….”
USIPOONA VEMA ni
tatizo maana KUSUDI linaendelea kujificha. Hii ni KANUNI ya kiroho. Ndio maana
anasema hapa “….HAZINA ZA GIZANI….” [ Zimefichwa sirini ili NONDO na KUTU visiweze kuharibu]. Ndio maana katika
Mathayo6;19-21 unaambiwa Jiwekeeni HAZINA Mbinguni [ NONDO, KUTU, wala WEVI
hawaibi ]. ANAKUTUNZIA MAHALI PA USALAMA maana yake bila kuwa na MACHO YA
ROHONI utakufa na hazina ziko palepale zilipohifadhiwa. Baada ya hapo watapewa
watu wengine.
Sambamba na neno la Warumi 12;2, “Wala msiifuatishe NAMNA(JINSI AU
MFUMO-STYLE) ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya NIA[ MAKUSUDI/MAWAZO
YA KIMAAMUZI] zenu, mpate kujua HAKIKA MAPENZI[ MAKUSUDI ] ya Mungu yaliyo
MEMA, ya kumpendeza, na UKAMILIFU”. Tunajifunza kuwa; kutofuatisha
NAMNA ya Dunia hii kunafanya NIA [MAKUSUDI] yako yageuzwe upya naweupate
kuyajua na kuendana na MAPENZI[MAKUSUDI] ya Mungu. Namna ya dunia katika;
kunena, kutenda, kuvaa, kula na kunywa, namna ya kutatua matatizo n.k.
UMUHIMU WA KUOMBA KWA
MZIGO ( MAOMBI MAZITO) YANAYOKUFANYA ULILINDE KUSUDI NA KUTEMBEA NDANI YAKE
1. MAOMBI YA YESU( 3 times in 3 hours)
-
Haya
maombi yalikuwa mazito kiasi cha kuachilia DAMU (UHAI) juu ya kile alichokuwa
anakitafuta (KUSUDI) kwa yeye kuwepo duniani la sivyo ANGELIPOTEZA KUSUDI. Luka
22;40-46.( Aliwaambia KESHENI msije mkaingia MAJARIBUNI)
TAMBUA; moja ya sababu za shetani kuachilia MAJARIBU (VISHAWISHI) ni KUKUTOA KWENYE
KUSUDI ULILOLIBEBA.
i.
MFANO
WA KWANZA; Isaka katika Mwanzo 25;29-34
ii.
MFANO
WA PILI; Yesu katika Luka 4;1- 4.
Katika mifano hii yote tunaona shetani akiwajaribu kwa
chakula katika kutaka kuwafanya wapoteze KUSUDI walilopewa na Mungu. Watu wengi
hutoka kwenye kusudi la Mungu kwa sababu tu ya chakula (hawataki maombi ya kufunga).
Lipo AGANO ambalo Mungu anataka alitimize kupitia wewe
kuwapo mahali Fulani. Usipokuwepo unakuwa unavuruga KUSUDI/RATIBA. Danieli 10;1
– 3,13, Danieli 9;1 – 27. Danieli baada ya kugundua kusudi la Mungu kumweka
pamoja na watu wake kule Babeli Anazama kwenye maombi mazito pasipo kujali
uwepo wa nyama nzuri wala chakula kitamu. Na kwa sababu anajua umuhimu wa lile
jambo anang’ang’ana mpaka pale Mungu anapojifunua kwake kupitia malaika.
Kuna mambo mengine yamkini unafanya uzembe katika kuomba ni
kwa sababu haujajua umuhimu wake kwako na kwa Mungu, laiti ungejua umuhimu wake,
hata radha ya chakula usingeikumbuka.
WAFAHAMU WATU NA KABILA ZA
WATU WANAOTOLEWA PUNDE UNAPOKUWA WA THAMANI(KUSUDI LINATEMBEA/LINAISHI) MACHONI
PA MUNGU
Isaya 43;4 biblia inasema, “ Kwa kuwa ulikuwa wa THAMANI machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, name
nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa WATU kwa ajili yako na KABILA ZA WATU kwa
ajili ya MAISHA YAKO(MLOLONGO MZIMA WA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU UKIWA
DUNIANI)”. Thamani yako kwa Mungu ni pale ambapo analiona kusudi
aliloliweka ndani yako LINAISHI, LINATEMBEA, LINAMLETEA FAIDA. Mungu anakuwa
anahangaikia kulipalilia kusudi ndani yako na moja kwa moja (automatically)
anakupalilia wewe. Hii ni kwa sababu wewe unakuwa chombo cha thamani ambacho
hakivujishi kusudi la Mungu. Kumbuka Kuharibika kwa chombo ndiyo kuharibika kwa
kilichobebwa.
Kumbuka nimekwambia Punda aliyekuwa amembeba Yesu Aliweza
kufunguliwa(kutolewa utumwa) na kupata heshima Ya kutandikiwa nguo na watu
wenye heshima zao kwa sababu alikuwa amelibeba kusudi la Mungu(amembeba Yesu
kama MFALME WA AMANI) vinginevyo angebaki hali ileile ya kufungwa. Mathayo 21;1
– 8.
Kwa mujibu wa kitabu cha Isaya 45;1-3 tunaona kuwa Unaposhikilia
kusudi la aliyekubebesha kusudi (MUNGU);-
i. MAPINGO YA CHUMA YANAKATIKA
o Kila kilichozuia njia yako kuelekea
mafanikio kinakatika
ii. MALANGO YANAFUNGUKA DAIMA
o Milango katika biashara, elimu, kazi,
watoto, mume au mke, kiroho na kiuchumi inafunguka.
iii. ANALEGEZA VIUNO VYA WAFALME
o Wafalme ni wale wenye mamlaka katika
eneo, shule,ofisi,wizara, nchi n.k. utapata upenyo kwao hata kama wengine
wanapita kupitia rushwa Mungu aliye mfalme wa wafalme anakupitisha kwao katika
jina la Yesu.
Maandiko yanasema katika Mithali 17;8, “Kipawa
[KUSUDI] ni kama KITO CHA THAMANI[ MADINI/MINERALS] kwake yeye aliye nacho;
Kila kigeukapo hufanikiwa”. KUGEUKA maana yake kufanya kazi
iliyokusudiwa na hicho kipawa.
NGUVU IFANYAYO KUSUDI LA
MUNGU KUDHIHIRIKA
(KUWA HALISI)
1.
Ni ile inayokuwa IMEHIFADHIWA ndani
yako
-
Efeso
3:20, “ Basi atukuzwe yeye awezaye
kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, KWA
KADIRI ya NGUVU ITENDAYO KAZI NDANI YETU”.
2.
Kiwango cha NGUVU unayohifadhi ndicho
kiwango cha juu (maximum) ambacho unaweza kukitoa[ The amount yo DEPOSIT is the
amount you CAN DRAW]
-
Isaya
37;3, “ Wakamwambia Hezekia asema hivi,
Siku hii ni siku ya dhiki, aibu na matukano; maana watoto (KUSUDI) wa tayari
kuzaliwa(KUDHIHIRIKA), wala hapana nguvu za kuwazaa(kufanya kusudi lidhihirike)”.
3.
Lazima kufahamu ni kiwango gani cha
NGUVU kinahitajika ili kufanya kusudi kudhihirika
-
Marko
8;22-25, “……………akamwekea mikono yake [kuachilia nguvu] , akamwuliza waona kitu?.
Akatazama juu, akasema, naona watu kama miti, inakwenda. NDIPO akaweka tena mikono yake( anaongeza kuvu
kufikia kiwango cha kutimiza kusudi) juu ya macho yake,………..akaona VYOTE
WAZIWAZI”.
4.
Unapobadilisha KANUNI(FORMULA)
umebadilisha MFUMO (SYSTEM) mzima
-
Kanuni
ya NGUVU ya Mungu ni kwamba ili iachiliwe lazima jambo inayokwenda kufanya liwe
linajenga ufalme wa Mungu au kwa lugha nyingine linatimiza mapenzi ya Mungu.
Yohana 15;16, “……………………..Nami nikawaweka mwende
mkazae matunda[ MAKUSUDI YA MUNGU]; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba
lolote mmwombalo Baba kwa Jina langu awapeni”.
MAMBO YATAKAYO KUSAIDIA
KULILINDA KUSUDI LA MUNGU
1.
Kuilinda imani
-
Uwe
kiroho mara nyingi zaidi ya kuwa kimwili (be more spiritual than social). Roho
inatazama zaidi ya jambo[beyond the matter] hii inakusaidia kutambua madhara ya
jambo Fulani kiroho juu ya kusudi ulilobeba hata kama kwa nje wewe au watu
wengine wanaliona liko vizuri halina shida. Ondoa[Omit ] mambo yote ya kimwili
(social) ambayo unayaona kuwa hayana msaada kiroho au yanayoathiri roho yako
kiimani.
1Yohana 2;15, “Msiipende dunia wala mambo(mabaya) yaliyomo katika dunia. Mtu
akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani,
yaani, tama ya mwili, na tama ya macho, na kiburi cha uzima havitokani na Baba,
bali vyatokana na dunia”.
2.
Fahamu umuhimu wa kujitenga umbali wa
kutupa jiwe
Isaya
55;8 – 9, “ Maana MAWAZO yangu (MAKUSUDI) si MAWAZO(MAKUSUDI) yenu, wala
NJIA(JINSI YA KUFIKIA KUSUDI) zenu si Njia zangu; asema BWANA……….”
Hapa anatujulisha
kuwa ushirika wako na Mungu ndio unaokufanya uwaze kama Mungu awazavyo na upite
NJIA ambayo Mungu anataka upite. Hivyo lazima uyajue kuwa kujitenga umbali wa
kutupa jiwe kimaombi kunakufanya;-
a.
Usisikie
mawazo au maoni ya mwanadamu juu ya maisha yako na kusudi la Mungu juu yako
badala yake umsikie Mungu na mawazo yake juu ya kusudi lake ndani yako
b.
Kuongeza
umakini na usikivu [CONCENTRATION] wakati Mungu atakapokuwa anasema nawe
c.
Kutafuta
WAZO JIPYA (to seek for the NEW IDEA) maana mawazo ya wanadamu ni mengi lakini
wazo la Mungu juu ya jambo Fulani ni moja tu.
Yesu
alifahamu umuhimu huu ndio maana mara nyingi ilikuwa lazima ajitenge na
wanafunzi ili atafute wazo la Mungu la siku. Jizoeshe kila siku kumwambia Mungu
kuwa naomba unipe WAZO JIPYA katika
maisha yangu, biashara, kazi, elimu, uchumi, kiroho, kifamilia, juu ya ndoa
yako, uchumba wako n.k
MWISHO
“ Nakutakia
mabadiliko na bidii kuu katika kulitafuta na kulilinda kusudi la Mungu maishani
mwako katika jina la Yesu . Usiwe mtu wa hasara hapa duniani,Mungu ajisikie
faida ya kukuumba wewe na kukuleta duniani na ufanikiwe katika mambo yote
katika jina la Yesu!! AMEEEN…!!!!!!!!!!!!!”
Somo hili limeandaliwa na;-
Mwalimu Nickson Kipangula wa Huduma ya
Maombi ya Urejesho.
Kwa maombi na maombezi, maoni na
ushauri au kama una swali lolote la Kiroho au kimaisha. Au unataka kuokoka au
kurejesha kwa upya uhusiano wako na Mungu. Tumia mawasiliano yafuatayo:-
Simu; 0757 35 05 27

Comments
Post a Comment