KUKUA KIROHO (SPIRITUAL GROWTH)



UNAPOKUA KUELEKEA UTU UZIMA KIROHO KUNA MAMBO KADHAA YATABADILIKA
 

Utu uzima ni wakati ambapo mambo mengi yahusuyo maamuzi utayaamua mwenyewe
Hautategemea wazazi kwa maamuzi yote
Hautategemea mchungaji wako kwa asilimia kadhaa
Utakuwa ndio kiongozi wa maisha yako (Hakuna wa kusema acha hiki au fanya hiki)
 

1. UNAFANYA MAAMUZI YA MAISHA YAKO MWENYEWE

Luka 1:80, Hapa tunaona kwamba yohana akiisha kukua alikwenda Jangwani. Hakuna mtu aliye mfuata huko na kumwambia fanya hiki au usifanye hiki. Alichokifanya ni kumsikiliza Mungu anasema nini? Hii ni sifa mojawapo ya kukua kiroho.Na hii ni kwa sababu alikuwa na nguvu za rohoni.
Muujiza wako unachelewa na yamkini ukafa kabisa kwa sababu hauna nguvu za rohoni.
Isaya 37:3, inasema, “Wakamwambia, Hezekia asema hivi, Siku hii ni siku ya dhiki, na aibu na matukano, maana watoto(MUUJIZA WAKO) wa tayari kuzaliwa, wala hapana nguvu(NGUVU ZA ROHONI) za kuwazaa”.

Unapokuwa huna nguvu ndani yako UTAHUBIRI, UTAIMBA, UTAOMBA lakini dhambi inakutafuna ndani kwa ndani. Hatari zaidi ni pale ambapo utaona aibu kuwaona watumishi wa Mungu ndiyo kufa kwenyewe. Unabaki na jina kuwa HAI wewe HALISI umekufa. Ni sawa na mtu aliyekuwa mwimbaji sasa sauti imekongoroka anaimbia CD watu wanajua sauti yake bado nzuri [PENDA KUIMBA LIVE WAKATI MWINGINE].Ufunuo 3:1-6

HAijalishi nin mchungaji, mwalimu, mwinjilisti, katibu wa maombi n.k unapokuwa umekamatwa na dhambi, shetani hakuachii kwa sababu una cheo (title) hiyo.Anaangalia kiwango cha nguvu ya MUNGU kinachoachiliwa dhidi yake.

Mungu anapokuonya uwe mwepesi kuelewa na kugeuka. “Hakuna atakaye kuonya tena kama utamkataa Mungu.

2.AINA YA MAOMBI UNAYOMBA INABADILIKA
Kuna namna tatu za kuwasilisha maombi kwa Mungu watu wanazitumia:
1. Kulalamika
2. Kudai/ Kukumbusha ahadi
3. Kuomba (KWA NEEMA)
Soma Habakuki 1:1-4, 2:1-4, 3:1-2.
Je, unatumia njia ipi/zipi kumfikia Mungu kwa maombi yako?

4. NAMNA YA KUFANYA MAAMUZI INABADILIKA
Wazo lolote linapokuja kwako utakuwa una lichuja akilini kwanza ndipo unaliachilia moyoni liendelee na mchakato wake. Kabla haujaliweka moyoni unamkabidhi Mungu kwanza alithibitishe/(proving)/ alifanyie uhakiki.Mithali 16:1-3.

Kama haujakuwa kiroho unapopokea wazo unalisokomeza ndani yako(MOYONI) kabla halijafanyiwa mchakato kwenye akili yako na haujamkabidhi Munngu alihakiki. Ndio maana unashindwa kuomba mambo mengine, kumshukuru Mungu au hata kuwaombea wengine.

Mambo mangapi yanakatiza (shortcut) kuingia moyoni mwako bila kupitia akilini. Mfano, tama ikiingia moyoni ni zinaa tayari, kuikamilisha kimwili inategemea na access ya mazingira.

5.LUGHA YAKO NA MAVAZI YAKO INABADILIKA

Vijisuruali vya kubana navijinguo vya Misri vinabadilika. Unavaa nguo za heshima (kukusitiri). Mtu haangaiki kujiuliza kuyu kaokoka au la!! 1Timotheo 2:9-10.
- Je, unakiri uchaji wa Mungu kwa kuvaa vijisuruali vinavyobana??
- Au kwa kuvaa vijinguo vinavyoonesha sehemu zisizo stahili??
- Au kwa kuvaa milegezo mpanka nguo za ndani zinaonekana??
Nikwambie “ huo ni utoto wa kiroho, inawezekana ukikua utaacha”.

6.UNAKUWA SIYO MTU WA KUOKOTEZA OKOTEZA
Unakuwa ni mtu wa kusubiri Mungu akupe vilivyo bora iwe mke/mume, mali, uchumi mafanikio ya kimaisha n.k. Mhubiri 6:9

MUNGU AKUBARIKI SANA

SOMO LITAENDELEA MUNGU AKIPENDA

Na: mwalimu Nickson Kipangula – R. P. S
Email: kipangulanickson@yahoo.com
Simu: 0757 350 527

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KURUHUSU UTUKUFU (GLORY) WA BWANA KUFANYA JAMBO KATIKA MAISHA YAKO