IBADA HALISI INAANZIA ROHONI
Yohana 4;23-24
IBADA ni ushirika kati yako na Mungu
sawasawa na nafasi zenu.
MAANA YAKE; Mungu ni baba yako na
wewe ni mwana wake. Hivyo, unanyenyekea na kusikiliza anachokuagiza baada ya
hapo unampa mahitaji yako.
>Yeye anakupa maagizo na
kusikiliza unachohitaji.( You MUST appreciate not only what God has done,but
also what he IS ABLE to do.
Katika Ibada halisi kuna:-
>Kuabudu halisi
>Imani halisi
>Ushuhuda halisi
>Maono halisi na,
>MIUJIZA halisi.
Bila kuzama rohoni mambo yako
yanakuwa ni ya kuigiza.
Warumi 8;5-6
·
Unalia machozi ya samaki baharini (yasiyokumbukwa)
·
Unapigana na upepo adui yupo upande
mwingine
*Wahubiri wengi huhubiri kwa hekima
za kibinadamu siyo kwa Roho mtakatifu na kwa NGUVU kwa kuwa Ibada zao si za rohoni.
1korintho 2;4-5
*Huwezi ukajua uliyokirimiwa na Mungu
(KARAMA ZA MUNGU KWAKO) kama hauabudu katika Roho na kweli. 1korintho 2;9-12
*Huwezi ukaabudu katika Roho na kweli
bila kuwa na Roho wa Mungu ndani yako. Galatia 5;25, Efeso 5;18
*Huwezi ukawa na Roho wa Mungu ndani
yako kama haujapewa uwezo wa kufanyika MWANA WA MUNGU(haujaokoka) .Yohana 1;14
Maombi na Neno ndio kiunganishi cha
wewe na Mungu kwa Ibada ya Rohoni.
>Maombi ni mawasiliano ya rohoni
kati yaw ewe na Mungu.MAANA YAKE:-Unaweza ukaingia kanisanin na kutoka bila
maombi ya Rohoni haujafanya Ibada halisi.
>>NDIO MAANA wengi huja
kanisani wakiwa wamebeba dhambi, matatizo, magonjwa n.k. na kurudi nayo
hivyohivyo.
>>Hata katika makanisa mengi
wanafuga mapepo, wachawi, majini, magonjwa na matatizo bila kujijua kwani ni
vitu vya rohoni na kuvitambua lazima kuwepo watu wa rohoni (wanaofanya Ibada
halisi)
Lazima ifike mahali kila mtu awe ni
mwombaji na si watumishi tu peke yao. Ndio maana watu wanahama hama makanisa
kwavsababu hakuna nguvu za rohoni zaidi ni porojo tu.Mungu atusaidie sana.
Nguvu za Mungu hazipatikani isipokuwa
tu kwa kuomba ,kufunga na kusoma Neno la Mungu.
Mfano; KATIKA MAHUSIANO, Kwa sababu
ya kutokuwa na Ibada halisi, watu wameingia KUTAMANI badala ya KUPENDA.
Mhubiri 6;9, “Heri kuona kwa macho(ya
rohoni) kuliko kutangatanga kwa tamaa(macho ya mwilini)……..”.
KUTAMANI – Macho ya nyama, sifa za
nje k.m urefu, weupe, wembamba n.k
KUPENDA – Macho ya rohoni, sifa za
ndani k.m utu wema, amani na watu wote, uvumilivu n.k. Galatia 5;22-23
Ukiambiwa nakupenda uliza kwa nini?
Akikutajia sifa za nje(MWILINI) ujue kuwa Hiyo ni TAMAA na wala si UPENDO.
‘’Bali utamkumbuka BWANA Mungu
wako……”. Kumbukumbu 8;18-20
>>Unaweza ukaomba mpaka
ukakonda lakini bila kujifunza IBADA HALISI utabaki maskini.
Hagai 1;5-7. Usifanye biashara ndani
ya nyumba ya Mungu(HEKALU) mahali pa Ibada yaani mwili wako.Warumi 12;1.utoe
mwili wako…….ndiyo ibada yako yenye maana.
Unapokaa na Mungu shetani hapati
kibali cha kukutesa. Isaya 35;8,10. Isaya 33;24.
>>Ndio maana hakuna utendaji
kazi wa NENO katika maisha ya watu.
>>Maisha yao ni tofauti kabisa
na kile wanachojifunza au kukisema makanisani.Hilo linaitwa (JINA LA KUWA HAI
LAKINI NDANI MFU).Ufunuo 3;1
--Unatakiwa uabudu mpaka uone NGUVU
ZA MUNGU zinashuka kiuhalisi kutoka juu. 2nyakati 5;13-14.
--Shetani kukuweza ni mpaka wewe
uache kuenenda kiroho badala yake uenende kimwili. 2korintho 10;3-5.
NAMWOMBA MUNGU AKUUMBIE MOYO SAFI WA
IBADA NA UWEZE KUMWABUDU YEYE KWA ROHO NA KWELI IBADA HALISI ITAKAYO KUBALIWA
NA BWANA KATIKA JINA LA YESU.
Na: mwl. Nickson Kipangula wa HUDUMA
YA MAOMBI YA UREJESHO
SIMU: 0757 35 05 27
EMAIL: kipangulanickson@yahoo.com
Website: www.urejesho.blogspot.com au
www.restorstionprayersservice.com
Comments
Post a Comment