IBADA HALISI INAANZIA ROHONI

Yohana 4;23-24
IBADA ni ushirika kati yako na Mungu sawasawa na nafasi zenu.
MAANA YAKE; Mungu ni baba yako na wewe ni mwana wake. Hivyo, unanyenyekea na kusikiliza anachokuagiza baada ya hapo unampa mahitaji yako.
>Yeye anakupa maagizo na kusikiliza unachohitaji.( You MUST appreciate not only what God has done,but also what he IS ABLE to do.

Katika Ibada halisi kuna:-
>Kuabudu halisi
>Imani halisi
>Ushuhuda halisi
>Maono halisi na,
>MIUJIZA halisi.

Bila kuzama rohoni mambo yako yanakuwa ni ya kuigiza.
Warumi 8;5-6
·         Unalia machozi ya samaki baharini (yasiyokumbukwa)
·         Unapigana na upepo adui yupo upande mwingine
*Wahubiri wengi huhubiri kwa hekima za kibinadamu siyo kwa Roho mtakatifu na kwa NGUVU kwa kuwa Ibada zao si za rohoni. 1korintho 2;4-5
*Huwezi ukajua uliyokirimiwa na Mungu (KARAMA ZA MUNGU KWAKO) kama hauabudu katika Roho na kweli. 1korintho 2;9-12
*Huwezi ukaabudu katika Roho na kweli bila kuwa na Roho wa Mungu ndani yako. Galatia 5;25, Efeso 5;18
*Huwezi ukawa na Roho wa Mungu ndani yako kama haujapewa uwezo wa kufanyika MWANA WA MUNGU(haujaokoka) .Yohana 1;14
Maombi na Neno ndio kiunganishi cha wewe na Mungu kwa Ibada ya Rohoni.
>Maombi ni mawasiliano ya rohoni kati yaw ewe na Mungu.MAANA YAKE:-Unaweza ukaingia kanisanin na kutoka bila maombi ya Rohoni haujafanya Ibada halisi.
>>NDIO MAANA wengi huja kanisani wakiwa wamebeba dhambi, matatizo, magonjwa n.k. na kurudi nayo hivyohivyo.
>>Hata katika makanisa mengi wanafuga mapepo, wachawi, majini, magonjwa na matatizo bila kujijua kwani ni vitu vya rohoni na kuvitambua lazima kuwepo watu wa rohoni (wanaofanya Ibada halisi)
Lazima ifike mahali kila mtu awe ni mwombaji na si watumishi tu peke yao. Ndio maana watu wanahama hama makanisa kwavsababu hakuna nguvu za rohoni zaidi ni porojo tu.Mungu atusaidie sana.
Nguvu za Mungu hazipatikani isipokuwa tu kwa kuomba ,kufunga na kusoma Neno la Mungu.
Mfano; KATIKA MAHUSIANO, Kwa sababu ya kutokuwa na Ibada halisi, watu wameingia KUTAMANI badala ya KUPENDA.
Mhubiri 6;9, “Heri kuona kwa macho(ya rohoni) kuliko kutangatanga kwa tamaa(macho ya mwilini)……..”.
KUTAMANI – Macho ya nyama, sifa za nje k.m urefu, weupe, wembamba n.k
KUPENDA – Macho ya rohoni, sifa za ndani k.m utu wema, amani na watu wote, uvumilivu n.k. Galatia 5;22-23
Ukiambiwa nakupenda uliza kwa nini? Akikutajia sifa za nje(MWILINI) ujue kuwa Hiyo ni TAMAA na wala si UPENDO.
‘’Bali utamkumbuka BWANA Mungu wako……”. Kumbukumbu 8;18-20
>>Unaweza ukaomba mpaka ukakonda lakini bila kujifunza IBADA HALISI utabaki maskini.
Hagai 1;5-7. Usifanye biashara ndani ya nyumba ya Mungu(HEKALU) mahali pa Ibada yaani mwili wako.Warumi 12;1.utoe mwili wako…….ndiyo ibada yako yenye maana.
Unapokaa na Mungu shetani hapati kibali cha kukutesa. Isaya 35;8,10. Isaya 33;24.
>>Ndio maana hakuna utendaji kazi wa NENO katika maisha ya watu.
>>Maisha yao ni tofauti kabisa na kile wanachojifunza au kukisema makanisani.Hilo linaitwa (JINA LA KUWA HAI LAKINI NDANI MFU).Ufunuo 3;1
--Unatakiwa uabudu mpaka uone NGUVU ZA MUNGU zinashuka kiuhalisi kutoka juu. 2nyakati 5;13-14.
--Shetani kukuweza ni mpaka wewe uache kuenenda kiroho badala yake uenende kimwili. 2korintho 10;3-5.

NAMWOMBA MUNGU AKUUMBIE MOYO SAFI WA IBADA NA UWEZE KUMWABUDU YEYE KWA ROHO NA KWELI IBADA HALISI ITAKAYO KUBALIWA NA BWANA KATIKA JINA LA YESU.

Na: mwl. Nickson Kipangula wa HUDUMA YA MAOMBI YA UREJESHO
SIMU: 0757 35 05 27
Website: www.urejesho.blogspot.com au www.restorstionprayersservice.com

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KURUHUSU UTUKUFU (GLORY) WA BWANA KUFANYA JAMBO KATIKA MAISHA YAKO