TOBA YA KUULETA
UFALME WA MUNGU ILI KURUHUSU MAPENZI YA MUNGU YA MBINGUNI YAFANYIKE DUNIANI
(sehemu ya 1)
Mathayo
4:17, “ …….tubuni maana ufalme wa Mbinguni umekaribia”.
TOBA – kubadilika
mtazamo, fikra, na mwenendo juu ya jambo baya ulilokua unalifanya ( changing
mindset and changing lifestyle from bad things to good things).
MWENENDO
– Tabia, maneno, mawazo na matendo
Kuna mambo
lazima ukubali kuyaacha unapotaka ufalme wa Mungu uingie ndani yako au mahali
ulipo ili Mungu atimize alilokusudia katika maisha yako.
Hatuokoki
tu kwa sababu tunataka kuingia mbinguni, tunaokoka ili tuunganishwe na nguvu ya
Mungu ya kutulinda na Yule mwovu tukiwa tungali duniani.
MAMBO AMBAYO MUNGU ANATULINDA
TUKIWA NA UFALME WAKE
Kazi ya
shetani ni kuiba, kuchinja na kuharibu Makusudi/mipango ya Mungu ndani yetu.
Kumbuka:
Ili Mungu afanye jambo Fulani kwako ni lazima akushirikishe.
Warumi 8:28,
“ Nasi twajua kuwa katika MAMBO YOTE Mungu hufanya kazi pamoja na wampendao
katika kuwapatia mema”.
Kwanza,
anaanza kuingiza WAZO ndani yako litakalofanya mawazo yasiyofaa ndani yako yaondoke. Isaya 55:8. Baada ya hapo
ndipo husema, “…NA TUFANYE….( gari, nyumba, ndoa nzuri, viongozi waadilifu, mtoto,
mume/mke n.k”) vitakavyo fanya huyu mtu awe na uwezo wa kuuendeleza ufalme
wangu duniani kwa kuzaa matunda.
Kuna
toba ya kukufanya uokoke maana yake upate kibali cha kuingia Mbinguni. Hii
inamhusu mtu binafsi
Kuna
toba iletayo ufalme wa Mungu duniani. Hii inamhusu mtu anayetubu, ardhi, anga
na watu wa ardhi katika eneo husika. Unapotubu kwa ajili ya ardhi ya eneo kwa mambo mabaya
yanayofanyika “baa, uzinzi, uchawi, ushirikina n.k” uwe na uhakika lazima mwana
wa Mungu( Yesu ) anadhihirika, hii ni kutokana na kuwa ufalme wa Mungu umeshuka
mahali hapo. Yesu anakuwepo kwa kazi kuu moja “AZIVUNJE KAZI ZA IBILISI”.
1Yohana 3:8b.
Ili uwe
ndani ya ufalme wa Mungu lazima ubadili mfumo wa maisha yako. Usiishi tena kama
MTUMWA, ishi kama MFALME. Automatically utajikuta unaacha kusema, “shetani
kajiinua” au “shetani alinipitia”.
UTUMWA
ni kufanya kitu ambacho haupendi kukifanya au kutoweza kufanya kitu ambacho
ulikuwa unapenda ukifanye. Wapendwa wengi leo hawapendi kuonekana Malaya,
wahuni, machangudoa, watu wa vijiweni n.k Lakini unapoangalia mavazi yao (
vijisuruali kwa wadada, vinguo vinavyoonesha maungo yao, mapambo na misuko ya
kikahaba, kurembua kimahaba, tattoo na pete zisizo na tafsiri [hayupo kwenye
uchumba wala ndoa], milegezo wakaka, mizaha na lugha za kihuni) utajua kuwa
wanatumikishwa na UFALME WA SHETANI. Aidha, wasingependa pia kuugua,
kuhuzunishwa, kupoteza wapendwa wao kishirikina, kupata ajali n.k. Vilevile
wapendwa wengi leo wangependa wawe wameshaoa/kuolewa, wana kazi, wanafaulu
masomo, wana mtoto, biashara zinafanikiwa, wana nyumba, kiwanja, n.k. Lakini
mpaka leo hawaoni uhalisia wa hayo yote. Shida nini??? UTUMWA!!!!
Biblia
inasema, “…………wala mtumwa hakai NYUMBANI siku zote; mwana hukaa nyumbani siku
zote. Basi MWANA akiwaweka huru mtakuwa huru kwelikweli”. Yohana 8;31-36.
Kumbuka:
hapa anazungumza na Wayahudi ambao tayari wamesha mwamini. Kwa leo tungesema
ambao WAMEOKOKA, tunakwenda sawa???
Sasa nisikilize:-
Anaposema mtumwa hakai nyumbani siku zote maana yake kuna wakati una tamani
ukae katika utakatifu, udumu katika mafanikio uliyonayo, usipatwe na matatizo
kutoka ufalme wa giza, ufaulu siku zote, ukae na ndoa inayodumu siku zote, uwe
na uchumba wa kudumu kukupeleka kwenye ndoa , lakini hauwezi inashindikana.
Shida nini?????? “ MTUMWA HAKAI NYUMBANI SIKU ZOTE” kumbuka hilo. Au haujawahi
kuona mabinti wengine ndani ya kanisa ambalo wamepatia wokovu, wanapoambiwa
hayo mavazi mf. Vijisuruali, vinguo vifupi, au night dress za mchana n.k hazikufai
wewe uliyeokoka jinsi wanavyopigana na hilo fundisho? Nakwambia huwa wanathubutu hata kuhama kanisa.
Wengine wakihubiriwa
juu ya sadaka, zaka na michango mbalimbali ya kanisa, husema tumechoka na
michango na wakati mwingine wanathubutu kuhama makanisa. Wakidhani bado wamo
ndani ya ufalme kumbe wanazunguka zunguka nje ya jengo (ufalme wa Mungu) . Inaniuma
sana hii.
“Mtumwa
hakai nyumbani siku zote” kuna muda anaachiwa achiwa, kuna muda adui
akichachamaa anambeba tena na kuondoka naye.
NGOJA TUONE MFANO HUU!!!!!!!
Mbuzi akiwa
amefungwa ili ale majani, huwa ni ngumu kujijua kuwa amefungwa, ni mpaka
anapotaka kwenda mbali zaidi ya ile kamba ndipo anapoona kamba inamzuia
(LIMITATION) lakini kabla, atafurahi, atacheza cheza na kuruka ruka kama
wenzake akijua yupo huru. Ila pale tu anapotaka kwenda BEYOND THE ROPE(Umbali
zaidi yahiyo kamba/kifungo) ndipo anapojua kuwa amefungwa, anaanza kulia,kujuta
na kuhuzunika. Anarudi tena kwenye usawa wa kamba anasahau kidogo machungu na
huzuni na anacheza tena na wenzake ( WALIOOKOKA ). Baadae anafikiri tena kwenda
BEYOND THE ROPE. Saa hii anatoka kwa spidi, ana hamu ya kula majani yaliyoko
beyond the rope; maskini yake anajikuta kamba ina mkaba kwa nguvu anaanguka,
kilio, huzuni na maumivu vimemjaa moyoni. Hatari zaidi aliyemfunga kamwona kuwa
anataka afanye mbinu za kwenda kula majani na ku enjoy kule beyond the rope,
anampa adhabu kali, viboko na mateke. Halafu anamrudisha tena anaendelea na
maisha yaleyale ya usawa wa kamba tena kwa mateso maana amemuudhi mfungaji.
Kwanini????MTUMWA HAKAI NYUMBANI SIKU ZOTE.
Haya ndiyo
maisha waliyoishi wana wa Israeli na tunaona pale Musa anataka kuwaondoa
utumwani, ndipo hasira ya Farao ikazidi, akawapa kazi ngumu zaidi na
kuwabebesha matofali ya moto. Kutoka 5:1-23. Lakini kwa uaminifu wa Mungu na
nguvu zake walipokuwa na utayari wa kukaribisha ufalme wa Mungu ndani yao
walifunguliwa kwa maana Bwana alikuwa ana haja nao wakaendelea na safari
kueelekea ukombozi na kusudi alilokuwa anataka wakalitimize.
Mwanapunda
aliyembeba Yesu alitambua kuwa alikuwa kwenye mateso na utumwa pale tu Yesu alipotuma
watu wakamfungue na kuwaambia waliomfunga BWANA ANA HAJA NAYE. Ufahari wa kutembea
juu ya nguo za watu na matawi ya mitende hakuwa nao kule kifungoni bali mateso
na kubebeshwa mizigo mizito kama waswahili wasemavyo “ PUNDA AFE MZIGO UFIKE”
Lakini pale tu alipo kubali kulibeba kusudi la ufalme wa Mungu la kumfikisha
Yesu Yerusalemu ndipo anaanza kuheshimiwa kama mwana na siyo mtumwa tena. Luka
19;29-36.
Ukiwa MWANA
unakaa nyumbani siku zote. Mwana ni Yule aliye mpokea Yesu. Yohana 1;12.
Kumpokea Yesu maana yake; kukubali mafundisho yake, watumishi wake na maonyo
yao, kukubali maisha yake (lifestyle) na kuukubali mfumo wa ufalme wa Mungu.
Yesu hasimami yeye kama yeye bali akisimama ujue ufalme wake upo. Na mtu pekee
atakayestahili kuwa ndani ya ufalme wake ni Yule aliye na utii na kufuata NENO
LAKE la sivyo, anakutoa nje ya ufalme. Kumbuka; ufalme una kanuni, taratibu na
sheria (BIBLIA).
Sasa
turudi kidogo; Ukiwa mwana wa Mungu maana yake umeubeba ufalme wa Mungu na
unachukua nafasi ya kifalme. Ufunuo 5;10, Luka 12;32. Katika kitabu cha Mhubiri
8;4 anasema, “….Neno la Mfalme lina nguvu ,naye ni nani awezaye kumwambia
wafanya nini?”. Kuna mambo utakuwa wewe ni kuamuru, hautaruhusu adui kufanya
bargaining. Mambo mengine siyo hata ya kumlilia Mungu kuwa kwa nini mimi.
Yaambie tokaaaa katika jina la Yesuuuu!!!!!!!haleluya!!
Watu wengi
wanapenda kuishi kwenye wokovu lakini hawataki kuishika sheria ya wokovu
(Sheria ya Roho wa Uzima) inayowafanya
wawe mbali na sheria ya dhambi na Mauti. Warumi 8;2. Ndiyo maana hupendi
dhambi lakini unatenda dhambi. Hupendi mauti ya ndoa, uchumba, kazi, elimu,
biashara, utakatifu, utumishi, huduma, karama n.k. itokee lakini unajikuta
mauti hiyo inakuandama. Kwanini????MTUMWA HAKAI NYUMBANI SIKU ZOTE. Lakini Mwana
akiwaweka huru, mtakuwa huru kwelikweli.
ITAENDELEA……………..!!!!
IMEANDALIWA
NA;-
Mwl.
Nickson Kipangula
HUDUMA
YA MAOMBI YA UREJESHO
(RESTORATION
PRAYERS SERVICE-WORLDWIDE)
SIMU: 0757
350527 (SMS NA WATSAPP)
EMAIL: nicksonkp@gmail.com
Blog: www.urejesho.blogspot.com
Comments
Post a Comment